Monday, April 09, 2012

NDEGE YA SHIRIKA LA ATC YAPATA AJALI MAPEMA LEO HUKO KIGOMA

Ndege ya shirika la ATC muda mfupi baada ya kupata ajali mapema leo mjini Kigoma.
Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wakitoka baada ya ajali.
Wananchi wakielekea eneo la tukio kutoa msaada.
Na mwandishi wa Tone Media
NDEGE ya Shirika la ATC ambayo ilikuwa imetoka  Dar es Salaam na kutua Kigoma salama na baada ya muda mchache kuanza safari ya kuelekea Tabora imepata ajali wakati ikijiandaa kupaa. Taarifa zaidi kutoka  kwa abiria ambao walikuwepo ndani ya ndege hiyo zinadai kuwa ilikuwa imejaza zaidi ya uwezo wake. Katika ajali hiyo bawa moja la upande wa kulia limevunjika kabisa na hakuna abiria hata mmoja aliyejeruhiwa vibaya. Hata hivyo kuna akina bibi wawili ambao wamepatwa na mshituko kutokana na ajali hiyo na wamekimbizwa moja kwa moja katika hospitali ya Maweni Kigoma.

CHANZO: KIGOMA YETU BLOG