Wednesday, April 25, 2012

Hongereni Chelsea kwa Kutinga Fainali -UEFA


 Mshambuliaji wa timu ya Chelsea,Fernando Torres akishangilia goli lake kwa hisia kali sana aliloipachikia timu yake dhidi ya Timu ya Barcelona katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la UEFA.kwa mche zo huu wa leo uliomalizika kwa suluhu ya bao 2 - 2,na kuifanya timu ya Chelsea kutinga hatua ya fainali.
Wachezaji wa timu ya Chelsea wakishangilia goli zuri lililofungwa mBrazil,Ramires (pili kulia) wakati wa mchezo wao uliomalizika muda mfupi uliopita dhidi ya timu ya Barcelona.timu hizo zimefungana Bao 2 - 2,lakini kutokana na bao 1 waliloshinda Chelsea katika mchezo wa awali imefanya matokeo kuwa Barcelona 2 - 3 Chelsea na kuifanya timu hiyo kutinga fainali bila zengwe.
Pamoja na kwamba Chelsea walicheza pungufu baada ya Nahodha wao,John Terry kulambwa kadi nyekundu,lakini waliweza kuhimili mchezo huo mpaka mwisho.
jirani leo hataki kuongea na mtu maana shunguli yake ishaishaaaa.......kufungwa noma jamaniii...