Wednesday, March 21, 2012

Mbashaz Flora and Emmanuel Kukutana Balozi Wa Tanzania Nchini

Wanamuziki wa Injili walio katika Nchi ya Marekani kwa ajili ya Gospel Tour Wameiambia Blog hii kuwa wanatarajia kukutana na Mhe. Balozi Mwanaidi Maajar ndani ya Ofisi ya balozi huyo baada kuona kazi ya Mbashaz ndani ya nchi ya Marekani. Balozi huyo ametoa appointment hiyo ili kuona namna gani Ofisi ya Balozi nchini Marekani inaweza kuwapa nafasi zaidi nchini humo kutangaza Utamaduni wa Tanzania kupitia Muziki wa Gospel ndani ya Marekani.
                                              Mbashaz Ndani ya Performance Nchini Marekani.


Flora pamoja na Emmanuel Mbasha wamezidi kufanya vizuri nchini Marekani ambako wako kwa ajili ya Ziara ya Muziki wa Injili nchini humo. Wakiwa wakiendelea kufanya matamasha hayo watu wengi wametokea kuwakubali hasa hasa na Sauti ya Ukweli ya Flora ambako huko wamekuwa na muda wa kitosha kufanya maonesho.


                                                                 Hakuna Kulala Marekani na Mbashaz.

Blog alipowasiliana na Mbashaz mambo yalikuwa namna hii.

Papaa: Mbashaz habari za huko Jamani?

Mbashaz: Safi kabisa Mungu ni mwema Papaa,

Papaa: Hivi Kweli nyie mtarudi huku maana naona mmekubarika sana huko Marekani kwa kazi yenu:

Mbashaz: Hahahaha Nyumbani ni Nyumbani kaka tupo kwenye Ziara then Tunarudi Nchini Kwetu tunamshukuru Mungu kwa Kibari ambacho Bwana ametupa:

Papaa: Kwa Kweli naona mko tight Mbaya, napenda kujua sasa mko wapi na mwelekeo ukoje.
                                                            Mamaa Flora Mbasha.

Mbashaz: Tulikuwa mji mmoja unaitwa Silver Spring Collage Park, kwa sasa tupo Washington DC kisha tunatazamia kwenda Virginia  siku ya Jumapili, wiki ijayo tunaenda Texas, Alabama, Carifonia kisha tutarudi Boston.

Papaa: Aaaah Mbashaz Mmetisha sana kwenye Next Level.

Mbashaz: Sifa na Utukufu Kwa Mungu.

Papaa: Kuna tetesi kuwa mmealikwa na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani.
                                            Mbashaz Akiwa na Papaa Mojawapo ya Matamasha ya Dar.

Mbashaz: Yes siku ya Ijumaa tunatazamia kukutana na Balozi kwa ajili ya Kikao kifupi.

Papaa: Nini hasa kusudi la Mwito huu.

Mbashaz: Kwanza ni kufahamiana lakini pia ni kuona namna gani Ubalozi unaweza kufanya kazi na sisi huku Nchini Marekani.

Papaa: Dhu Next time naomba mnibebe kama mwandishi wenu aiseee.

Mbashaz: Sawa Papaa.

Papaa: Nawatakia Ziara Njema.

Blog itaendelea kuwapasha habari zaidi.


Kwa hisani ya Sam Sasali a.k.a Papaa