Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli kushoto , akizungumza na Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa ibada hiyo leo.
Dk. Harrison Mwakyembe wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya
pamoja na baadhi ya wabunge, kushoto ni Mbunge wa Same Mashariki
Mama Anne Kilango Malecela, Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na
Mbunge wa Kahama Bw. James Lembeli.
Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lilloko Kawe Tanganyika
Pakers akimkaribisha Dk Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na Naibu
Waziri wa Ujenzi katika ibada iliyofanyika leo kwenye kanisa hilo na
kuhudhuriwa na Waziri wa Afrika Mashariki mzee Samwel Sitta na baadhi ya
wabunge kadhaa, Mzee Samwel Sitta amesema Mwakyembe amekwenda kanisani
hapo ili kutoa ushuhuda kuhusu ugonjwa wake kwa ujumla ambapo
FULLSHANGWE ilishuhudia tukio hilo.
Dk. Harrison Mwakyembe ametoa ushuhuda akimshukuru mungu kwa kumbariki
na kuendelea kumpa nguvu juu ya afya njema, Mwakyembe ambaye alikuwa
amevalia kofia na Glovu katika mikono yake, ameongeza kwamba tangu
alipokuwa ameondoka kwenda nchini India kwa matibabu Oktoba 9 mwaka jana
hakuwahi kuvaa viatu, lakini leo amevaa, hivyo akamshukuru mungu kwa
miujiza yake.
Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akiongea katika ibada hiyo na
kumkaribisha Dk Harrison Mwakyembe ili kuzungumza machache na waumini wa
kanisa hilo na kutoa ushuhuda wake.
Dk Harrison Mwakyembe akishuka katika madhabahu mara baada ya kumalizika kwa ibada hiyo leo.
Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akishuka katika madhabahu mara
baada ya kumalizika kwa ibada leo.Picha zote kwa hisani ya Fullshangwe