Hapa na Pale Katika Maisha
Jeremiah Sumari.
Habari zilizotufikia asubuhi hii zinasema kuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jeremiah Sumari amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Habari zinasema kuwa mbunge huyo aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kwenye ubongo kwa muda mrefu.
Imeelezwa kwamba kuna kipindi hali yake ilikuwa mbaya ambapo alipelekwa kutibiwa nchini India. Baada ya kupata matibabu, alirudishwa nchini ambapo amefariki saa 8 usiku wa kuamkia leo akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtandao huu unatoa pole kwa wote waliofikwa na msiba huu!