Watafiti Wasaidizi na Wasimamizi wa Utafiti
Kipima-rushwa AFRIKA MASHARIKI (EABI)
Ndugu,
Jukwaa la Uwazi Tanzania (TRAFO) kwa kushirikiana na TI-Kenya, TI-Uganda, TI-Rwanda and TI-Burundi linakusudia kufanya utafiti juu ya hali ya rushwa katika nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EABI). Utafiti unafanyika nchini Tanzania sambamba na Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, na unatarajiwa kuanza April 14, 2011. Kama ilivyokuwa mwaka jana, utafiti utafanyika katika ngazi ya kaya kwenye nchi zote za Afrika Mashariki.
Ili kutekeleza hilo, ForDIA imepewa jukumu la kuratibu ajira za watafiti wasaidizi wasiopungua 40 kutoka Tanzania Bara na Visiwani kufanya utafiti huo katika maeneo yanayopendekezwa kwa mujibu wa sampuli nasibu. Aidha, tunakusudia kuajiri Wasimamizi wa Utafiti wanne (4) watakaoratibu na kusimamia shughuli za mradi katika nagzi ya kanda. Kipaumbele kitatolewa kwa watafiti wasaidizi na wasimamizi wenye uzoefu, hususan walioshiriki EABI mwaka jana (2010). Aidha, tutatoa kipaumbele kwa wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja na watafiti wasaidizi wenye uzoefu kutoka asasi washirika wa utafiti wa mtazamo rushwa (CPS) watakaokuwa tayari kushiriki EABI 2011. CPS ni mradi unaoendeshwa na ForDIA kila mwaka.
Sifa za watafiti wasaidizi
1. Elimu: Angalao kidato cha sita.
2 Uzoefu: Uwezo wa kuwasiliana, kuandika ripoti.
3. Ukaazi: Mkazi wa eneo la kufanyia utafiti
4. Wasaa: Kuwa na wasaa na utayari wa kuwepo kwenye eneo la utafiti wakati wote wa kazi
Sifa za Wasimamizi wa Utafiti (Kanda)
1. Shahada ya elimu ya juu katika sayansi ya jamii kutoka chuo kikuu kinachotambulika kisheria.
2. Utayari na uwezo wa kusafiri katika mikoa yote iliyomo katika Kanda
3. Uzoefu wa kusimamia/ kuratibu utafiti
Muda wa utafiti
Utafiti utafanyika kwa siku kumi (10) kwa watafiti wasaidizi, na siku kumi na tano (15) kwa Wasimamizi wa utafiti. Mikataba yote itasainiwa baina ya TI-Kenya na watafiti watakao ajiriwa. Mikataba itazingatia, pamoja na mambo mengine, posho na pesa za kujikimu wakati wa utafiti. Aidha, watafiti wasaidizi na wasimamizi watalipwa pesa ya usafiri wa kila siku. Ikiwa kutakuwa na ulazima, wasimamizi wa utafiti watalipwa posho za malazi; lakini si kwa watafiti wasaidizi.
Jinsi ya kuomba: Tuma barua ya maombi na CV yako (kupitia njia ya barua pepe) kwa:
EABI Coordinator;
Tanzania Transparency Forum (TRAFO)
Off University Road, Survey Area, Kawe/Mlalakuwa Plot # 301-304, House # 250
P.O. Box 32505, Dar es Salaam –TANZANIA
Tel: +255 22 2701890, +255 22 2701895-6, Cell: +255 784 410 939
Fax: +255 22 2701890
E-mail: TRAFO@fordia.org or info@fordia.org
Mwisho wa kutuma maombi: 09 Aprili, 2011