Bi Maghimbi alisema, ameamua kujiengua na chama hicho kwa kuwa viongozi wa juu wanaendelea kuilea rushwa ndani ya chamda hicho
Alisema chama hicho kimetawaliwa na rushwa kupita kiasi na ziliweza kukithiri katika uchaguzi wa kura za maoni.
Alisema katika kampeni hizo kuwa yeye ni mwanasiasa mkongwe ambako alikua ndani ya chama hicho kwa muda mrefu lakini alishindwa kupambana na rushwa ndani ya CUF kwa kuwa viongozi walikuwa wakiilea.
Alidai ndani ya chama cha CUF wanawake wamekuwa hawapewi nafasi ya kugombea uongozi na kuteuana kwa kupitia rushwa jambo ambalo limeonekana kumkera
Bi. Fatma Maghimbi, alikuwa msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, na aliweza kuwa mbunge wa Chake Chake, Pemba katika kipindi cha miaka 10 tokea mwaka 1995.