Monday, October 11, 2010

Number +3588976578 bado inaendele kutuma ujumbe wa kizushi.

Hawa jamaa wanamatatizo gani mbona wanaendelea kutuma msg yao. Wewe unayefanya hivyo kama umetumwa na hao jamaa koma ukomae. Upuuzi wako peleka kwa hao hao, toka umepata uhuru mlikuwa wapi kufanya vyema nanyi mngepata kibali? Sasa matope hadi kwenye simu

Nilipata tena SMS ambayo inazungumzia kuhusu ya Uchaguzi kuwa mwenye chama fulani hafai kuwa Rais.


Maoni yangu:
  1. TCRA wanaitambua hii number au imesajiliwa nchi gani?
  2. Huyu alietuma hiyo msg mbona hajajitambulisha kuwa yeye ni nani?
  3. Pia unatumia kigezo gani kuwa hafai kuwa Raisi kama sio uongo ni nini?
  4. Kuna shule ya kusomea Urais?
Mimi kwa mtazamo wangu kijana kajianze upya na mambo yako hayo ya kutumia msg watu bila utambulisho na umetumwa na nini?

Ewe mwanablog hii mchunie huyo jamaa na piga kura kwa mtu anayeweza kuleta Maendeleo nchi yetu achana na ushabiki.