Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege ya uchukuzi ya jeshi la angani la nchi hiyo imeanguka kaskazini mwa jimbo la Sumatra.
Wanasema kuwa tayari miili 20 zimepatikana katika eneo la ajali.
Maafisa wa kijeshi nchini Indonesia, wanasema kwamba ndege hiyo ya uchukuzi ya majeshi ya taifa hilo, ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani.
Ndege hiyo ya kubeba mizigo aina ya Hercules ilikuwa na wahudumu 12 na abiria 50 ilipoanguka.
Kuna ripoti kuwa watu bado wanasikika wakipiga mayowe katika majengo yaliyoanguka.
Ndege hiyo iliharibu kabisa nyumba ambayo iliangukia katika mji wa Medan, kaskazini mwa jimbo la Sumatra.
Picha za runinga na kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moto unatoka kwenye mabaki ya ndege hiyo.
Msemaji wa jeshi la angani alisema kuwa rubani alikuwa ameomba kurejea katika uwanja wa kambi ya kijeshi kwa sababu ya matatizo ya kimitambo.
BBC.