Ni matumaini yangu kuwa nyote muwazima na sie hatujambo huku Bondeni Sauzi.
Maudhui ya barua hii ni kukufahamisheni kuwa kuna Mtanzania kwa jina Shukuru Goyagoya kafariki tarehe 16th mwezi huu katika Hospitali ya Baragwana Jo'burg.
Alikua Kalazwa ICU takriban mwezi mmoja.
Hapa Sauzi alikuwa akiitwa kwa jina la umaarufu Jastice Mliambe Manesi kazaliwa mwaka 1970.
Maelezo niliyoweza kupata, Mama yake mzazi anaitwa Bi Ziada Musa Kitima anaishi Mabibo CCM . Naomba msaada wenu wa kutangaza katika chombo chako habari hii ili jamaa zake marehemu taarifa hii iweze kuwafikia popote pale walipo. Na taarifa hii nimeweza kuifikisha katika Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria
Mpaka sasa maiti bado ipo Hospitalini tunasubiri uamuzi wa pamoja ikiwa marehemu azikwe hapa Jo'burg au maiti yake isafirishwe hadi nyumbani kwao. Nashukuru kwa msaada
Wenu. Kila la kheri
Omar Mutasa
BBC
Joburg