Friday, July 04, 2014

TACAIDS yakutana na wanahabari jijini dar



TACAIDS yakutana na wanahabari jijini dar
Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela.
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika banda la TACAIDS kwenye viwanja vya Sabasaba jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa.
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela kati akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Ufuasihii wa dawa na huduma za jamii wa ICAP Globali Health Action Bi: Agnes Rubare Rwegasha alipotembelea banda la ICAP, kushoto ni Afisa Mawasiliano Kutoka TACAIDS Bw. Godlease Malisa.
Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dr. Jerome Kamwela akimuuliza swali Mwelimisha Rika kutoka PSI (Population Service International) Bi: Veronica Mbilinyi alipotembelea banda hilo katika Viwanja vya Sabasaba leo jijini Dar es Salaam. (Picha na: Genofeva Matemu)