Friday, July 04, 2014

Airtel Divas yatembelea kikundi cha Sauti ya walemavu kwenye Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba


Airtel Divas yatembelea kikundi cha Sauti ya walemavu kwenye Maonyesho ya Biashara ya Sabasaba
Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania 'Airtel Divas', Meneja wa Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi (kushoto), Afisa Uhusiano, Jane Matinde (wa pili kushoto), na Afisa mauzo, Rachael Mboya (kulia), wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, walipotembelea Banda la Swauta, lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana. Airtel Divas ilikiwezesha kikundi hicho, kupata pesa kwa ajili kulipia banda hilo.
Mwanachama wa Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, Adelina Mluge (kulia), akitoa maelezo kuhusu bidhaa zinazouzwa na kikundi hicho kwa Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania 'Airtel Divas', (kutoka kushoto), Afisa Mauzo, Rachael Mboya, Afisa Uhusiano, Jane Matinde na Meneja wa Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi, walipotembelea Banda la Swauta, lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana. Airtel Divas ilikiwezesha kikundi hicho, kupata pesa kwa ajili kulipia banda hilo.
Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania 'Airtel Divas', Meneja wa Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi (kulia), na Afisa Uhusiano, Jane Matinde (kushoto), wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, walipotembelea Banda la Swauta, lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana. Airtel Divas ilikiwezesha kikundi hicho, kupata pesa kwa ajili kulipia banda hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na kikundi SWAUTA katika banda lao kwenye maonyesho ya Sabasaba, ambapo Airtel Divas imekiwezesha kikundi hicho kuwa na banda katika maonyesho hayo.
Afisa Mauzo wa Airtel , Rachael Mboya,akiangalia kazi ya kikundi cha ulemavu ikiwemo kushona na uwezo wa kusoma vitabu mbalimbali vilivyopo katika banda lao wakati wanawake wa Airtel Divas walipotembelea banda lao katika maoenyesho ya sabasaba.

Umoja wa kikundi cha wanawake cha Airtel Divas leo kimetembelea kikundi cha sauti ya wanawake walemavu Tanzania (SWAUTA) katika banda lao lililopo katika maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Saalam

Airtel Divas wamefanya hivyo hivyo ikiwa ni muda mfupi tu tangu walipofanya harambee ya kukiwezesha kikundi hicho kupata fedha za kulipia banda katika viwanja vya maonyesho ya 38 ya kimataifa maarufu kama Sabasaba ili nao kuonyesha bidhaa zao kwa watanzania

Akiongea wakati wa ziara hiyo, mwanachama wa Umoja wa wanawake wa Airtel na Meneja Huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema" Airtel Divas tunayofuraha kuona tumeweza kuwasaidia kina mama wenzetu kutimizia lengo lao na kuwapa nafasi yakuweza kuonyesha ubunifu wao uwezo wao na kazi zao za mikono kwa washiriki na wateja wa ndani na wanje wanaotembelea maonyesho haya ya Sabasaba.

Ni matumaini yetu kuwa fulsa hii ya kuonesha na kujitangaza hapa saba saba itawawezesha kufikia malengo yao ya kutanua wigo wa biashara zao na kupata masoko na kuuza bidhaa zao kwa wingi zaidi. Tunatoa wito kwa watanzania kujitokeza na kuwaunga mkono kina mama hawa katika banda lao lililoko Benjamini Mkapa.

Kwa upande wake Mwanachama wa Umoja wa sauti ya walemavu Tanzania Bi Adelina Mluge Alisema "Tunawashukuru sana Airtel kwa kutuwezesha kuwepo katika mazingira mazuri ukilinganisha na ilivyokuwa na miaka iliyopita. mpaka sasa tumeweza kupata wateja wengi wakipita hapa kuona na kununua bidhaa zetu kwa wingi. Tunategemea kufanya vyema katika maonyesho ya mwaka huu kutokana na maboresho haya na hivyo basi tunaishukuru sana kampuni ya Airtel kwa kujitolea kutusaidia.

Airtel kupitia huduma zake za jamiii imeweza kuwafikia jamii na kuwawezesha kupata huduma muhimu hususani katika elimu, Airtel kwa kupitia Divas Airtel inaendelea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo kina mama hawa wa umoja wa sauti ya walemavu Tanzania.