Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania kuanzia leo imezindua huduma mpya ya kuwarahisishia wateja wake maisha ambayo ni ya usajili wa wateja wapya wanaonunua line za simu kwa njia ya kieletronikia.
Huduma hii ya usajili wa wateja wapya kwa njia ya kielektronikia inachukua nafasi ya usajili wa kujaza fomu uliokuwepo hapo awali na imeonekana kuwa ni bora na ya haraka na inapunguza kazi ya kujaza karatasi na kupunguza uwezekano wa taarifa za mteja kupotea na wateja wametokea kuifurahia.
"Wanachotakiwa kufanya wateja wanaonunua line za mtandao wetu ni kututembelea duka lolote la wakala wetu wakiwa na vitambulisho vyao na picha zao za muonekano wa sasa,hakuna sababu ya kuingia gharama za kutoa nakala ya kitambulisho kama ilivyokuwa hapo awali"Anasema Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Usajili wa line za simu kielektronikia unawahusu wateja wapya wanaojiunga na mtandao wa Vodacom na wateja wa zamani ambao wanatumia mtandao na usajili huu unafanyika kwa mujibu wa maelekezo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).Vodacom imebuni mfumo huu kuondoa usumbufu wakati wa zoezi la kujisajili ikiwemo kuokoa muda na gharama na pia imeona ini muhimu kuwa na mfumo wa kudumu rafiki wa kusajili watejawanaoendelea kujiunga kwenye mtandao wake.
"Wateja wetu tunawapa umuhimu wa kwanza,hivyo tutaendelea kuboresha huduma zetu.Maendeleo haya yanatuwezesha kuwa na mtizamo wa kuwapatia huduma na bidhaa bora siku zote".Ameongeza Meza.