JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb), amemteua Dk. Steve Mdachi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), kuanzia tarehe 03 Juni, 2016.
Kufuatia uteuzi huo, amewateua pia wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PBPA kuanzia tarehe 03 Juni, 2016.
1. Dkt. Daniel Sabai
2. Dkt. Henry Chalu
3. Dkt. Siasa Mzenzi
4. Mr. Salum Mnuna
Imetolewa na;
KATIBU MKUU
6 Juni, 2016