Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza leo limeng'oa kwenye wadhifa
wake Meya wa Jiji hilo Bw.Josephat Manyerere(CHADEMA) kutokana na madai
ya wajumbe wa baraza hilo kupitia barua walioiwasilisha Mei 24 mwaka huu
iliyokuwa ikimtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo kuitisha kikao cha dharula
ili kumsomea Meya mashitaka yake.
Madiwani
waliojiorodhesha na kufikia theluthi mbili ya wajumbe wapatao 17 kati ya
wajumbe 33 wakiwa halali wa vikao vya baraza la madiwani wa Jiji hilo
ambalo ilidai ni suala la kisheria na kanuni ya 80 za kudumu za
halmashauri hiyo ambayo ipo wazi na inasomeka .
“Halmashauri
inaweza kumuondoa Mwenyekiti au Meya madarakani kwa azimio linaloungwa
mkono na theluthi mbili ya wajumbe kutokana na sababu yoyote ya sababu
hizo ni (a) Kutumia nafasi yake vibaya(b),Kushiriki vitendo vya
rushwa(c),Kushindwa kazi(d),Mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu na(e)
lemavu wa kimwili aidha kiakili kwa kiasi cha kumfanya kushindwa
kutekeleza majukumu yake kama Mwenyekiti ama Meya.”ilifafanuliwa kanuni
hiyo.
![]() |
Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe. |
Baada ya
kukubalika kwa hoja hiyo Mkurugenzi Bw.Kabwe aliwataka wajumbe wasiyo wa
kikao hicho cha Kamati kutoka nje ya ukumbi huku viongozi waalikwa
waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo,RAS Bi
Dorothy Mwanyika na Wakuu wa wilaya za Nyamagana Bw.Baraka Konisaga na
Bi.Amina Masenza wakitakiwa kubaki kwa mujibu wa taratibu za
Halmashauri.
Hatimaye baraza lilirejea kama kawaida yake baada ya kusikiliza utetezi wa Meya Bw.Manyerere ambapo katika madai kumi yaliyowasilishwa ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili kusomewa naye kujitetea kisha ukafanyika uamuzi wa kumpigia kura za wajumbe ili kumuondoa madarakani aidha kumuacha aendelee na nafasi yake ya Umeya.
Naibu Meya wa Jiji hilo Bw.Charles
Chichibela(CHADEMA) ambaye ni Diwani wa Kata ya Mahina alitangaza
matokeo ya kura hizo za wajumbe kama ifuatavyo alisema kwamba idadi ya
wajumbe waliohudhulia kikao hicho wapatao 28 kati ya 33 ambao ndiyo
halali lakini kutokana na wengine kuwa katika majukumu mengine ya
kitaifa.
![]() |
Bwana Josephat Manyerere, Meya aliyetemwa na madiwani wa jiji la Mwanza kupitia kura za kutokuwa na imani naye hapa ilikuwa awali kabisa akiendesha kikao hicho kabla ya 'kuvulishwa joho'. |
![]() |
Bwana Josephat Manyerere, Meya aliyetemwa na madiwani wa jiji la Mwanza kupitia kura za kutokuwa na imani naye akitoa neno la mwisho nmara baada ya 'kuvulishwa joho'. |