Majibu ya Serikali:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika mahojiano yake leo, Alhamisi, Aprili 5, 2012, na Redio One, ikiwa
ni kauli yakeya kwanza baada ya Mahakama Kuu ya Arusha kutangaza kumvua
ubunge, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bwana Godbless Lema, amedai
kwa jazba sana kuwa hukumuya Mheshimiwa Jaji Gabriel Rwakibalira
imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Ikulu.
Kauli hii ya Bwana Lema ni upuuzi. Siyo Mheshimiwa Rais Kikwete wala
Ikuluimeingilia kati kesi yake kwa namna yoyote ile, iwe ni kwa kupiga
simu amakuzungumza na Mheshimiwa Jaji Rwakibalira.
Kwa hakika, haijapata kutokea Mheshimiwa Kikwete, tokea alipoingia
madarakani, Desemba 21, 2005, akaingilia, kwa namna yoyote ile, mwenendo
wa kesi yoyote ile katika Mahakama yoyote na ya ngazi yoyote katika
Tanzania. Na wala hakusudii kufanya hivyo wakati wote wa muda wake
uliobakia wa uongozi. Siyo kazi ya Rais kutoa hukumuama kuelekeza namna
ya kutoa hukumu katika kesi zilizoko Mahakamani. Rais hana madaraka wala
mamlaka hayo.
Aidha, kauli ya Bwana Lema ni ukosefu mkubwa wa adabu na heshima kwa
Mahakamaambao ni Muhimili Huru usioingiliwa na Serikali ama na Muhimili
mwingine katikamaamuzi yake. Bwana Lema amekuwa kiongozi kwa muda sasa,
hivyo ni lazimaatambue jambo hili kubwa na muhimu katika mfumo mzima wa
utawala wa nchi yetu.
Ni jambo lisilokuwa na mshiko wala tija, na kwa kweli ni bahati mbaya,
kwamba BwanaLema anajaribu kuingiza mambo yasiyohusika katika jambo la
dhahiri kabisa kuwa ni lakisheria ambalo msingi ni hoja na maelezo
mahakamani.
Bwana Lema asitafute visingizio kwa yaliyomfika kwa sababu hakuna mtu
mwingine wakumbebea msalaba huu. Badala ya kutafuta mchawi asiyekuwepo,
ni vyema Bwana Lema angekaa chini na kuangalia ni sababu zipi za
kisheria zilizomfanya ashindwe na kama ameridhika kuwa hakutendewa haki
akate rufani kwa mujibu wa sheria na taratibu. Tunaomba wananchi
wampuuze. Ameshindwa kesi kwa makosa yake aliyofanya hanamtu wa kumlaumu
bali ajilaumu mwenyewe.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
05 Aprili, 2012
Source: Jamii Forums