Sunday, September 28, 2014

WADAU GASTO NA FEDERICA WAMEREMETA JIJINI ARUSHA



WADAU GASTO NA FEDERICA WAMEREMETA JIJINI ARUSHA
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Gasto Leseiyo akiwa ame 'pose' kwa picha na Bibi harusi Federica Sikale baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro Arusha jana na kufatiwa na sherehe iliyofanyika ukumbi wa Leons Garden Sakina.
Gasto Leseiyo na Mke wake Federica Sikale baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Ngarenaro Arusha wakiwa katika picha ya pamoja na Mama wazazi .
Bwana harusi Gasto Leseiyo akisalimia wageni kwenye ukumbi wa Leons Garden,Sakina jijini Arusha akiwa na Mke wake Federica Sikale baada ya kufunga pingu za maisha.
Bwana harusi Gasto Leseiyo na Mke wake Federica Sikale wakiwa na wapambe wao Endrick Fredick(shoto) na Lucy Fransis(kulia) kwenye ukumbi wa Leons Garden Sakina.
Bwana harusi Gasto Leseiyo na Mke wake Federica Sikale wakijumuika kusakata muziki na ndugu zao waliohudhuria sherehe hiyo.