Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
Mmoja wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Susan Nakawuki (mwenye blauzi ya pinki) akinunua bidhaa kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
: Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki akiwemo Mhe. Shyrose Bhanji anayewakilisha Tanzania katika bunge hilo wakiangali kazi za sanaa ya uchingaji kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji wa Tanzania akimkabidhi zawadi ya sinia lililotokana na kazi za uchongaji Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margareth Zziwa mara baada ya kupenda bidhaa hiyo na kuamua kumnunulia spika huyo jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).
Katikati ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa Mhe. Makongoro Nyerere (katikati) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afika Mashariki wa Serikali ya Tanzania Bibi. Joyce Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel walipokuta katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi hiyo. Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari.Vijana, Utamaduni na Michezo.