Thursday, May 15, 2014

UGOMVI WA MAKANISA WAMALIZWA NA MUJATA MBEYA

 

Kushoto askofu Fredrick Silumbwe na askofu Anyimike Mwakalasya wakikumbatiana kuashiria kumalizika kwa mgogoro

Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Chifu Shadrack Merere akitoa nasaha zake katika mapatano hayo

Askofu Fredrick Silumbwe

Askofu Anyimike Mwakalasya

 

Waumini wa pande zote mbili

 




Waumini wa Makanisa ya PCGT(Pentecoste Church of God Tanzania)linaloongozwa na Askofu Anyimike Mwakalasya na PEWOMI(Pentecostar World Wide Ministries)linaloongozwa na Askofu Fredrick Silumbwe wamemaliza mgogoro uliokuwa Mahakamani na kudumu miaka mitatu bila muafaka.

Mgogoro huo umetatuliwa na Asasi isiyokuwa ya kiraia ya Muungano wa Jamii Tanzania(MUJATA)na kuridhia kufuta kesi iliyokuwa Mahakamani bila masharti yoyote ikihusisha pande hizo mbili baada ya waumini hao kutishiana kuuana na kujengeana chuki kwa muda mrefu.

Mapatano hayo yamefanyika mbele Viongozi wa MUJATA akiwemo Mwenyekiti Soja Masoko,Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Chifu Shadrack Merere na wajumbe wanne wa wanawake ambapo pande hizo mbili ziwekeana saini mkataba wa kumaliza mgogoro.

Ugomvi wa waumini hao ulitokana na kuvuliwa madaraka kwa Askofu Fredrick Silumbwe hivyo yeye kuamua kuanzisha Kanisa jipya la PEWOMI hali iliyowafanya baadhi ya waumini kuwekwa mahabusu hali iliyozidisha machafuko na kuchochea chuki miongoni mwa waumini.

Na Mbeya yetu