Maadhimisho hayo yanataraji kufanyika Juni 5 mwaka huu, chini ya uratibu wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kabla ya zawadi na Tuzo hizo kutolewa na ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.
Hida aliwataka wataalamu na watendaji wa Jiji hilo kujiandaa na maadhimisho hayo, ambapo tayari ofisi ya Waziri Mkuu imeisha toa vigezo vya kushindaniwa na Majiji, Manispaa na Halmashauri za wilaya nchini kote.
" Watendaji wa Kata na Mitaa tuendelee na mkakati wetu wa usafi kwenye Kata na Mitaa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi ili jiji hilo liibuke tena na tuzo ya ushindi kwa mara ya tisa mfululizo," alisisitiza
Mkurugenzi Hida alisema juzi kwamba, "Tutumie sheria ndogo ndogo za Hamashauri yetu na kuhamasisha wananchi na vikundi vya usafi kuweka mazingira katika hali ya usafi kabla ya wakaguzi kupita kwenye Mitaa na Kata kutoa maksi." Alieleza.
Aidha alifafanua kwamba, pia katika maadhimisho hayo jiji linategemewa kupata wageni kutoka Majiji, Miji, Manispaa na Halmashauri za Wilaya za ndani na nje ya nchi, ambao wamekaribishwa kushiriki katika maadhimisho hayo.
Huku akitamba kunyakua ushindi kwa mara ya tisa, Hida aliwaagiza maafisa afya wa jiji hilo kuweka mikakati ya kuendeleza usafi katika jiji hilo aliloliita Smart City ili kuwa kivutio kwa wawekaezaji na wageni watakaokuja.
Kwa upande wake, Meya wa Jiji hilo Stanslaus Mabula amemtaka Mbunge wa jimbo la Nyamagana Ezekia Wenje aache kuwachochea wafanyabiashara ndogondogo (machinga) na kuwachonganisha na viongozi wa serikali na Jiji ili wavunje taratibu, kanuni na sheria za Mipango miji.
Meya, Mabula akihutubia Baraza la Madiwani wa jiji hilo, alisema kwamba licha ya Wenje kutoshiriki mara kwa mara vikao vya baraza hilo, lakini amekuwa akiwahamasisha wamachinga na wafanyabiashara wengine kufanya biashara katika maeneo wasiyo ruhusiwa jambo ambalo linaweza kusabaisha jiji hilo lipoteze ushindi.
"Kwa hili niwaombe wafanyabishara wanaofanya biashara katika maeneo yasiyo ruhusiwa ikiwa pamoja na wanaopanga bidhaa nje ya maduka na sehemu za wapiti kwa miguu, waache mara moja kwani wanavunja sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kifungu namba 187 (1) na 191 Act Cap 20/2004." Alisema.