Friday, May 23, 2014

ANATAFUTWA NA NDUGU ZAKE

 
 
 
 
Salaam aleikum Ankal na timu nzima ya Globu ya Jamii,

Msaada tutani Ankal, kuna anko wetu amepotea (pichani hapo). jina lake Amir Husein Binyaga ni mkazi wa Kiluvya amewahi kuishi Tanga majani mapana ana umri wa miaka 56 alipotea tangu tarehe 15/05/2014 saa 12 asubuhi hadi leo familia bado inamtafuta taarifa zipo kituo cha Polisi Kibaha, maili moja. Taarifa zozote tutapokea kupitia namba 0754322317 0754273711,0653768329,0718260177.

Shukrani.