Hizi ni chochoro ambazo wakazi hao wa milimani wanazitumia kupita huku zikiwa zimejazana mawe ambayo kwa mujibu wawenyeji mawe hayo yanahatarisha sana usalama wa watu wanoishi chini ya milima kwasababu mvua zinaponyesha nyingi huwa yanaporomoka.
Kama haujaangalia vizuri unaweza kudhani ni jengo moja refu la ghorofa lakini si hivyo ila ujenzi wa milimani jijini Mwanza, hapa ni kwenye eneo la Kata ya Isamilo ipo ubavuni mwa jiji hilo upande wa kaskazini. Mbali ya kuwa ni mlimani lakini si milima hivi hivi ila ni milima yenye mawe makubwa na madogo ambapo hata ujenzi wake ni wachangamoto nyingi sana.
Hapo ndipo kwenye soko la mtaa huo ambapo wakazi wake huenda kupata mahitaji muhimu.
Hapo bondeni kidogo kuna Shule ya Sekondari ya Daniel Ole Njolai.
Hiki ni kimoja ya aina ya vyoo vinavyojengwa, ni mawe yaliyounganishwa na tope la udongo ambapo mvua ikinyesha unaporomoka chini.
Lakini kando ya eneo hilo wapo wanapiga matofali ya udongo ili kubadilisha aina hiyo ya ujenzi wa mawe ambao ni mgumu kwa watu wasio na kipato cha kuweza kununua saruji ya kujengea.
Ukiwa juu kabisa kwenye eneo la Mtaa wa Nyakabongo C, unaweza kuona vizuri zaidi mandhari ya Jiji la Mwanza kama inavyoonekana pichani.