Mmoja kati ya washiriki wa shindano hilo akionyesha uwezo wake katika kuonyesha kipaji chake
Baadhi ya washiriki na watazamaji wa shindano hilo wakiwa ukumbini leo
Mwandishi wetu Denis Mlowe anaripoti kutoa mkoani Iringa kuwa ,Jitihada za mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) katika kuhamasisha michezo mbali mbali kwa vijana wa jimbo la Iringa mjini zimeendelea kuzaa matunda baada ya leo kutekeleza ahadi yake ya kuanzisha mashindano ya kuibua vipaji kwa wasanii hao.
Katika shindano hilo la kutafuta vipaji kwa awamu ya kwanza katika mkoa wa Iringa limeonyesha kuwa na mvuto mkubwa kwa wakazi wa Manispaa ya Iringa ambao wamejitokeza kwa wingi ukilinganisha na makisio ya kuwa na washiriki wachache zaidi .
Shindano hilo la Kabati katiba star search limefanyika kwa mafanikio kwa vijana wengi wenye vipaji kujitokeza na kuonyesha vipaji vyao katika ukumbi wa hallfear mjini hapa.
katika shindano hilo wasanii wengi vijana waliweza kuimba mbela ya majaji Eddo Bashir(Ebony Fm) Temmy Mahondo wa radio country fm, dj Ammy Yeyo( Country fm )Agnes Anderson(ebony Fm na Dj Muba wa radio Ebony Fm huku majaji hao wakionyesha kutoamini kutokana na umahiri wa wasanii hao.