Thursday, August 16, 2012

MATOKEO NA JINSI MECHI YA TAIFA STARS NA BOTSWANA ILIVYOKUA.

.
Picha ya liblary.
 
Matokeo ya Taifa Starsna Botswana kwenye mechi iliyochezwa jana ni 3-3 ambapo mpaka kwenye  mapumziko game ilikua 2-2.
Stars ilikua ya kwanza kupata goli kupitia kwa Erasto Nyoni dakika ya 17 kwa njia ya penalty iliyotokana na mwamuzi kutoa adhabu baada ya beki Oscar Obuile wa Botswana kumuangusha Mrisho Ngasa.
 
Botswana walisawazisha dakika ya 26 kupitia kwa Lemponye Tshireletso nje ya eneo la hatari kumshinda nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja lakini dakika tano baadae Mwinyi Kazimoto aliifungia Stars goli la pili kwa shuti la mbali pia.
 
Tshireletso aliisawazishia tena Zebras dakika ya 37 Mfungaji alifunga bao hilo kwa kichwa lakini Mrisho Ngasa aliipatia Stars goli la mwisho kwenye dakika ya 84 baada ya kushirikiana vizuri na  Simon Msuva.