29 Julai, 2012 - Saa 17:36 GMT
Kumezuka mabishano nchini
Uingereza kuhusu viti vitupu kuonekana kwenye mashindano kadha ya
Olimpiki siku ya Jumamosi, pamoja na mashindano ya beach volleyball,
gymnastics na mashindano ya awali ya kuogelea.
Inafikiriwa viti hivo vitupu ni vile vilivotengwa kwa ajili ya wakuu, wafadhili, wanariadha na waandishi wa habari.
Mwandishi wa BBC anasema swala la tikiti ni tete, kwa sababu washabiki wengi wa Uingereza walitaka kununua tikiti wakaambiwa zimekwisha.
Source:BBC