Sunday, July 29, 2012

Jeshi la Uganda laingia Congo


 29 Julai, 2012 - Saa 17:16 GMT

Mashirika yasiyokuwa ya serikali katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, yanasema kuwa wanajeshi wa Uganda wameingia Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, kupigana pamoja na jeshi la huko dhidi ya wapiganaji waitwao M23.

Wanajeshi wa DRC walioingia Uganda kuwakimbia M23
Mashirika hayo yanasema magari ya deraya sita, yaliyojaa wanajeshi yamevuka mpaka kutoka Uganda, na kuingia jimbo la Kivu Kaskazini.
Jeshi la Uganda limekanusha tuhuma hizo.
Mataifa kadha ya magharibi yamesimamisha msaada kwa Rwanda, baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kusema kuwa Rwanda inalisaidia kundi la wapiganaji la M23 -- tuhuma ambazo zinakanushwa na Rwanda.

Source:BBC