Saturday, July 28, 2012

Ebola yazuka tena Uganda

 28 Julai, 2012 - Saa 17:24 GMT

Baada ya tetesi za majuma kadha, serikali ya Uganda na Shirika la Afya Duniani, WHO, wamethibitisha kuwa ugonjwa wa Ebola umeibuka magharibi mwa nchi.
Virusi vya Ebola
Watu kama 13 wamekufa na wengine kadha wanauguwa ugonjwa huo katika wilaya ya Kibaale.
Chanzo cha ugonjwa huo safari hii kingali kinachunguzwa.
Virusi vya Ebola havina dawa wala chanjo ya kinga, na kati ya ishara zake ni homa, kutapika, na kuhara.
Ugonjwa huo ulizuka Uganda miaka 12 iliyopita, na kuuwa watu zaidi

Source:BBC