Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa, Juma Nyoso (kushoto) na John Boko, wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mafisango kuupeleka sehemu iliyopangwa.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania wakiwasili TCC Chang'ombe.
Vilio na majonzi vilisikika leo asubuhi katika viwanja vya TCC Chang’ombe, jijini Dar es Salaam, wakati maelfu ya waombelezaji walipojitokeza kuuaga mwili wa mchezaji wa timu ya Simba, Patrick Mutesa Mafisango, aliyefariki usiku wa kuamkia jana alfajiri kwa ajali ya gari maeneo ya Chang’ombe jijini.(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY, RICHARD BUKOS, GPL)