Shirikisho la soka nchini Tanzania , TFF, limemsimamisha kazi msemaji wake Florian Kaijage
baada kushindwa kupiga wimbo za taifa wakati wa mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya afrika kati
ya Morocco na Tanzania .
Kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambapo Rais kikwete alikuwa mgeni rasmi, baada ya kukagua
timu na kusubiri nyimbo za taifa, hakuna kilichosikika zaidi wapenzi wa Yanga kuanza
kuimba "Mungu ibariki Yanga".
Mpaka sasa bado haijafahamika kwanini nyimbo hizo zilishindwa kupigwa. Kufuatia kitendo
Mpaka sasa bado haijafahamika kwanini nyimbo hizo zilishindwa kupigwa. Kufuatia kitendo
hicho, TFF imeamua kumsimamisha kazi msemaji wa TFF, Florian Kaijage mpaka hapo uchunguzi
utakapokamilika.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni na michezo,
Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni na michezo,
wanaunda kamati itakayochunguza chanzo cha tatizo hilo huku Kaijage akiwa nje mpaka uchunguzi
utakapokamalika.
Lakini katika hatua nyingine Tenga amesema ndani ya mwezi mmoja TFF inatarajia kutangaza nafasi
Lakini katika hatua nyingine Tenga amesema ndani ya mwezi mmoja TFF inatarajia kutangaza nafasi
mbili za ajira zilizoachwa wazi, ambazo ni ya sasa ya Msemaji wa shirikisho hilo na ile ya Katibu wa
TFF ambapo awali ilikuwa ajira ya Frederick Mwakalabela ambaye alijiengua ili kugombea Ubunge
wa Iringa Mjini (CCM).credit: Jane John blog