Friday, May 27, 2016

Waziri Mahiga apokea msaada wa magari ya kubebea wagonjwa kutoka Korea Kusini


Waziri Mahiga apokea msaada wa magari ya kubebea wagonjwa kutoka Korea Kusini

Waziri wa Mambo ya nje Ushirikano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (aliye shikilia funguo za gari), akipokea Ufunguo wa Magari ya Wagonjwa kutoka kwa Balozi wa Korea Kusini nchini, Mhe. Song Geum Young yaliyotolewa Serikali ya nchi yake. Waziri Mahiga alitumia nafasi hiyo Kuishukuru na kuipongeza Serikali ya Korea Kusini kwa msaada huo ambo utatumika kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza. Tanzania na Korea Kusini zina mahusiano mazuri, ambapo Korea Kusini inaendelea kuisaidia Tanzania kwenye sekta mbalimbali zikiwemo afya,miundombinu, elimu na uchumi. 
Waziri Mahiga akijaribisha moja ya magari aliyokabidhiwa na Serikali ya Korea Kusini kupitia Balozi Young kushoto. 
Picha ya Magari yaliyotolewa kwa msaada wa Serikali ya Korea Kusini.
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Korea Kusini Mhe. Song Geum Young mara baada makabidhiano ya magari kwa Mhe. Dkt. Mahiga (hayupo pichani).Picha na Reginald Philip