Wednesday, November 25, 2015

UNESCO YAELEZEA MATUKIO YA WAANDISHI WA HABARI TAKRIBAN 700 KUUAWA



UNESCO YAELEZEA MATUKIO YA WAANDISHI WA HABARI TAKRIBAN 700 KUUAWA
SHIRIKA la kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) limeeleza kuwa waandishi wa habari takriban 700 wameuawa katika kipindi cha miaka 10, huku zikionyesha wastani kuwa kila baada ya wiki moja mwandishi mmoja anauawa duniani.

Pia ilisema kwa mujibu wa ripoti ya waandishi wasio na mipaka kuhusu matukio ya uhuru wa waandishi wa habari, Tanzania imeshuka kwa nafasi sita ambapo hapo nyuma ilikuwa nafasi ya 69 kati ya nchi 180 kati ya mwaka 2006 mpaka 2014, lakini kwa mwaka 2015 ipo katika nafasi ya 75.

Akizungumza katika mkutano uliowajumuisha wataalamu wa habari, jijini Dar es salaam, Mwakilishi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues, alisema asilimia 94 ya waandishi hao ni wale wa ndani ya nchi na kwa vyombo vya habari vikubwa ambapo chache kwa waandishi wa kigeni.

Alisema kutokana na matukio hayo, ilichochea kwa UNESCO kufatilia na kujua tatizo kubwa na kuandaa agenda chini ya Umoja wa Mataifa(UN) ili waandishi waweze kuwekewa usalama katika maeneo yao ya kazi.

"UNESCO tulilaani vitendo hivi na tuliweza kusikiliza kesi takribani 540 za waandishi, pamoja na kutafuta chanzo cha tatizo hili na njia ya kuweza kuliondoa," alisema Zulmira.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na wandishi wa habari (hawapo chani) juu ya waandishi wa habari takriban 700 waliouawa katika kipindi cha miaka 10, huku zikionyesha wastani kuwa kila baada ya wiki moja mwandishi mmoja anauawa duniani, katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel, akifafanua jambo katika mkutano huu ulio fanyika leo jijini Dar es Salam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel,akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa habari walio fika katika mkutano huo ulio fanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.