Friday, May 22, 2015

MREMA: WALIODAI KUNIENGUA UANACHAMA TLP WALISHAWAFUKUZWA


MREMA: WALIODAI KUNIENGUA UANACHAMA TLP WALISHAWAFUKUZWA


MBUNGE wa Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, Mhe. Agustino Lyatonga Mrema amesema kuwa kamati ya maridhiano iliyodai imemvua uanachama haikuwa halali kwa kuwa wanachama wake akiwemo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Joram Kinanda walishafukuzwa tangu Mei 7, mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari leo, (Alhamisi) katika Ukumbi wa Habari Maelezo uliopo Posta jijini Dar es Salaam, alisema kamati hiyo ni ya wahuni na inatumiwa na wanasiasa wanaolitaka jimbo hilo na si wanachama halali wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP).

"Kamati ya Kinanda si halali kwa sababu haina mamlaka ya kunifukuza kwa mujibu wa katiba lakini pia naviomba vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa weledi na siyo kwa ushabiki wa kisiasa na kama vitafanya hivyo vitaipeleka nchi pabaya,'' alisema Mrema.