Wednesday, April 01, 2015

HISTORIA FUPI YA KABILA LA WA ARUSHA



HISTORIA FUPI YA KABILA LA WA ARUSHA

Waarusha ni kabila linalopatikana kaskazini mwa Tanzania katika eneo la mlima MeruMkoa wa Arusha. Lugha yao ni Kiarusha inayotazamiwa kama lahaja yaKimaasai Wakati wa kuja kwa wakoloni hao walikuwa wakazi wa eneo la mji wa Arusha wa leo.




Kwa namna yoyote katika eneo la mlima Meru Waarusha walikuwa majirani wa karibu na Wameru wanaosema lugha karibu na Wachagga. Wameru waliwahi kufika Meru mapema wakakalia sehemu za juu zaidi mlimani wakati Waarusha walianza chini zaidi.  Mwanzoni walipigana kati yao lakini baadaye walianza kushirikiana kwa karibu hadi 1881 Wameru walikaribishwa kuunga vijana wao katika rika mpya ya Waarusha iliyoitwa "talala".

Asili ya Waarusha

Kuna mawazo mawili juu ya asili ya Waarusha.
Wengine wanasema asili yao ni kundi la Wamaasai walioshindwa katika vita kati ya Maasai na hivyo kutafuta kimbilio kati ya wakulima; walianza kulima wenyewe na hivyo kutofautiana na Wamaasai wengine.
Wengine wanasema asili yao ni Wapare waliohamia mlima Meru kufuatana na mapatano na Wamaasai. Hapa walianza kutumia lugha ya Wamaasai na kupokea desturi nyingine. Wakati wa sotoka kubwa ya 1892 Wamaasai ambao mifugo yao walikufa wote walijiunga na Waarusha na hivyo kuimarisha athira ya kiutamaduni ya Kimaasai kati yao.waarusha walitokea meru.


Zamani ya ukoloni

Katika miaka ya 1880 wakoloni wajerumani walianza kufika katika eneo la Kilimanjaro kati ya Wachagga. Wakati ule Waarusha walikuwa wakishirikiana na machifu wa Wachagga katika vita zao. 
Waarusha waliathiriwa sana na uvamizi wa ugonjwa wa sotoka wa 1892 ulioua asilimia kubwa ya ng'ombe nchini. Wakidhoofishwa vile Wakoloni Wajerumani walianza kufika wakajaribu kutawala maeneo.
Wajerumani waliingia polepole katika eneo la mlima Meru. Mara ya kwanza Waarusha walikutana nao mwaka 1881 wakati ambako kundi dogo la Wajerumani chini ya Hermann von Wissmann pamoja na Wachagga wa Moshi na kundi la Waarusha walishambulia Kibosho; 1885 walishambuliwa na Wajerumani kutoka Moshi chini ya Kurt Johannes kama kisasi kwa mashambulio yao dhidi ya makabila yaliyoshirikiana na Wajerumani.
1896 Ovir na Segebrock, wamisionari Wajerumani Walutheri waliuawa na vijana Waarusha; kapteni Johannes alirudi na askari zake na kundi kubwa la Wachagga na kuharibu nchi ya Waarusha na Wameru mara mbili katika 1896 na 1897