Tuesday, April 14, 2015

CHARLES HILLARY ATUA RASMI AZAM TV


CHARLES HILLARY ATUA RASMI AZAM TV
Mtangazaji Charles Hillary akiwa ndani ya studio za Azam TV.


MTANGAZAJI mahiri Charles Hillary aliyekuwa Shirika la Habari la BBC jijini London leo ametua rasmi katika kituo cha Television cha Azam TV kuungana na watangazaji wenzake.
Katika tasnia ya habari, Charles Hillary amefanya kazi ya utangazaji kuanzia mwaka 1980 hadi mwaka 1993 akiwa Radio Tanzania Dar es Salaam.
Mwaka 1994 alijiunga na Radio One ikiwa ni radio ya kwanza binafsi kuanzishwa nchini Tanzania.
Mwaka 2003 aliamua kuacha kazi Radio One na kujiunga na Radio DW Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani ambapo alifanya kazi mjini Koln na baadaye Bonn hadi mwaka 2006 alipokatiza mkataba wake baada ya kupata ajira Idhaa ya Kiswahili ya BBC London ambako alijiunga tarehe Aprili 14, 2006.