Wednesday, March 25, 2015

Watu sita wafariki baada ya basi la Super Shem kugongana uso kwa uso na gari la halmashauri Nzega



Watu sita wafariki baada ya basi la Super Shem kugongana uso kwa uso na gari la halmashauri Nzega
Watu sita wamefariki Dunia na wengine tisa kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari manne likiwemo basi la kampuni ya Super Shem lililokuwa likitokea jijini Dar-es-salaam kuelekea mkoani Mwanza majira ya saa sita usiku ambapo liligongana uso kwa uso na gari ya halmashauri ya wilaya ya Nzega na kusababisha magari mengine mawili kugongana baada ya kukosa muelekeo.

Ajali hiyo imetokea katika barabara ya Mwanza – Dar-es-salaam eneo la kijiji cha Undomo kata ya uchama wilayani nzega mkoani tabora.

  Katika ajali hiyo  inayodaiwa kuwa chanzo chake ni mwendo kasi na baadhi ya madereva katika magari hayo kutokuwa makini ambapo basi la Super Shem lenye nambari za usajiri T874 CWE lililokuwa likitokea Dar-es-salaam liligongana uso kwa uso na gari aina ya LAND CRUIZER lenye nambari za usajiri SM 4905 mali ya halmashauri ya wilaya ya nzega ambapo watumishi watatu wa halmashauri hiyo walifariki dunia. 

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Bw.Patrick Mbozu anaeleza namna walivyopokea tukio hilo la ajali lililosababisha majonzi na simanzi Kaimu mganga mkuu mfawidhi wa wilaya ya Nzega Dr.Erick Mbuguye anaeleza hali ya majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo na kulazwa.

 Miili ya marehemu iliyotambuliwa ni pamoja na aliyekuwa dereva wa gari la halmashauri Charles  Sanga,mhasibu wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Bw.Emmanuel  Kasenyi,Bwana afya wa wilaya Peter  Steven,Robert Kisabho mtumishi wa halmashauri,Yasinta  Alex mkazi wa isunga  na matukuta  malikita.