Wednesday, January 28, 2015

BUNGE LAAHIRISHWA BAADA YA VURUGU KUHUSU POLISI KUWASHAMBULIA WAFUASI WA CUF



BUNGE LAAHIRISHWA BAADA YA VURUGU KUHUSU POLISI KUWASHAMBULIA WAFUASI WA CUF

Mbunge wa NCCR–Mageuzi, James  Mbatia.

Baada ya James Francis Mbatia kuleta hoja ya dharura juu nguvu iliyotumiwa na polisi dhidi ya maandamano ya CUF jana, ili ijadiliwe na wabunge kama hoja ya dharura, Spika Makinda aliamuru serikali ilete majibu kesho ndipo ijadiliwe. 

Wabunge walisimama kushinikiza hoja ijadiliwe lakini Makinda aliendelea na msimamo wake wa hoja kujadiliwa kesho baada ya serikali kuleta majibu.  Hapo ndipo sintofahamu ilipozidi na kuleta kutoelewana kati ya wabunge wa upinzani na spika na Ilibidi spika aahirishe bunge mpaka kesho lakini baadaye akabadili na kusema litarejea saa kumi jioni leo.