Sunday, August 31, 2014

LIVERPOOL YAUA 3-0 BALOTELLI AKIANZA



LIVERPOOL YAUA 3-0 BALOTELLI AKIANZA
Liverpool imeng'ara leo kutoka kulia Sturridge, Gerrard na Balotelii
LIVERPOOL imeichapa mabao 3-0 Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa White Hart Lane.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya nane kwa shuti la umbali wa mita saba, Steven Gerrard dakika ya 48 kwa penalti baada ya Eric Dier kumchezea rafu Joe Allen na Alberto Moreno dakika ya 60.
Mshambuliaji mpya, Mario Balotelli aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan wiki iliyopita, leo amecheza mechi yake ya kwanza Liverpool, lakini hakufunga licha ya kucheza soka nzuri.
Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Moreno, Gerrard, Lovren, Sakho, Henderson, Sterling/Enrique dk86, Sturridge, Balotelli/Markovic dk61 na Allen/Can dk61.
Tottenham Hotspur: Lloris, Dier, Rose/Davies dk72, Capoue, Kaboul, Vertonghen, Lamela, Bentaleb/Dembele dk59, Adebayor, Eriksen/Townsend dk59 na Chadli
CHANZO BIN ZUBERY


ROONEY ATIMIZA MIAKA 1O AKIWA MCHEZAJI WA MAN UNITED




ROONEY ATIMIZA MIAKA 1O AKIWA MCHEZAJI WA MAN UNITED

Muongo mmoja: Wayne Rooney (kulia) ametimiza miaka 10 tangu asajiliwe Manchester United kutoka Everton Agosti 2004
MSHAMBULIAJI Wayne Rooney leo ametimiza miaka 10 tangu asajiliwe na Manchester United kutoka Everton.
Rooney amepata mafanikio ya kuridhisha akiwa na United, ikiwemo kushinda mataji matano ya Ligi Kuu, moja la Ligi ya Mabingwa, moja la Klabu Bingwa ya Dunia na mawili ya Kombe la Ligi.
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Seri Alex Ferguson  kwa Pauni Milioni 25 Agosti 31, mwaka 2004 amefunga mabao 218 katika mechi 444 ndani ya miaka yake 10 kwenye klabu hiyo na sasa amepewa Unahodha na kocha mpya, Louis Van Gaal.


RACHAEL CLAVERY ASHINDA TAJI LA MISS LAKE ZONE 2014. AONDOKA NA MKOKO WA MILIONI 10!




RACHAEL CLAVERY ASHINDA TAJI LA MISS LAKE ZONE 2014. AONDOKA NA MKOKO WA MILIONI 10!
Mshindi wa Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Mary Emanuel( kulia) na Mshindi wa tatu Nikole Sarakikya ( kushoto). Rachael amejinyakulia zawadi nono ya Gari la millioni 10 CCM Kirumba Jijini Mwanza. Shindano hilo lililokuwa na Walimbwende 18 wote wakichuana vikali kila mmoja akitaka ashinde hatimaye usiku huu Rachael Clavery amewafunika wenzake na kuibuka na ushindi. Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com
Kwenye picha ya pamoja

Kwenye picha ya pamoja washindi
 
Mshindi wa Miss Lake Zone 2014, Rachael Clavery
Doreen Robert (kushoto) Aliyeshika nafasi ya nne akipata picha ya pamoja na wenzake.
Gari aliloshinda Miss Lake Zone 2014 Rachael Clavery usiku huu...
Mshindi wa kwanza alizawadiwa gari ya shilingi mil 10, mshindi wa pili alijibebea bajaji yenye thamani ya sh. mil 4 huku mshindi wa tatu alijipatiapatia pikipiki ya Tsh mil 1.8

Jaji Mkuu wa shindano hilo, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga ambao ndio waandaaji wa Miss Tanzania akitangaza tano bora.
Walioshika nafasi tano bora
Wakiulizwa maswali.
Viongozi mbalimbali
Warembo wakiwa katika Vazi la Ufukweni
Warembo wakiendelea na Vazi la Ufukweni
Doreen Robert(kulia) akipita na mwenzake na Vazi la Ufukweni
Warembo hao walikuwa wamepiga kambi ya siku 10 katika Lenny Hotel ya Mkoani Geita na walichuana kuwania taji lililokuwa linashikiliwa na Ruth Charles.

Dada wakiwaangalia wadogo zao
Wadau wakichukua kumbukumbu..
Msanii wa Kizazi kipya Barnabas akitumbuiza mashabiki
Barnabas akiimba wimbo wake live na kundi la Sky Light Band jukwaani.
Kundi zima la Skylight Band likishusha muziki mkali

Skylight Band wakifanya yao jukwaani..
Meneja wa bendi ya Skylight, Anneth Kushaba a.k.a AK 47 akifanya yake jukwaani.
Meneja wa bendi ya Skylight, Anneth Kushaba a.k.a AK 47 akizungusha zungusha huku akiweka mbwembwe juu ya jukwaa CCM Kirumba kwenye mashindano ya Miss Lake Zone 2014.
Mgeni rasmi Leonard Bugomola Mkurugenzi wa Lenny Hotel ambaye pia alikuwa mmoja wa wadhamini wa Shindano hilo akizungumza na Wakazi wa Mwanza waliojitokeza katika Uwanja wa CCM Kiumba juu ya swala zima la Miss Lake Zone 2014. 

Mratibu wa shindano la Miss Lake Zone 2014, Flora Lauwo (kushoto) akiwa na Mgeni rasmi Bw. Leonard Bugomola. Pia Mratibu aliongeza kuwa Wakiwa kambini wilayani Geita, warembo hao walifanya shughuli za kijamii ikiwemo kutoa msaada kituo cha Yatima cha Moyo wa Huruma na kutembelea mgodi wa GGM na Hospitali ya Geita na Hifadhi ya Lubondo na kufanya usafi.

Mratibu huyo ametoa pongezi kwa wadhamini wakuu, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji cha Redd's, Lenny Hotel, Crown Paint, Shule ya Rishor Pre & Primary English Medium na Benki ya CRDB ya Geita. Picha na Faustine Ruta wa bukobasports.com

Warembo wote 18 jukwaani
Vazi la ufunguzi..warembo wote 18 walipanda jukwaani
Warembo waliopanda jukwaani ni Mikoa yao kwenye mabano ni Moshy Shaban: Doreen Robert; Christina Jilulu (Mwanza): Nikole Sarakikya, Mary Emanuel na Rachael Julika (Shinyanga).
Wengine ni Faudhia Haruna, Jackline Kimambo na Christina John (Kagera), huku Nyangi Warioba: Cecilia Kibada na Everlyn Charles (Simiyu). Wamo pia Martina John: Elinaja Nnko, Winfrida Nashon (Mara)huku Rose Msuya, Rachael Clavery na Faridha Ramadhani wakiwakilisha mkoa wa Geita.


TRA NA JESHI LA POLISI WATOA ONYO



TRA NA JESHI LA POLISI WATOA ONYO
 Bw. Rished BADE, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akiongea na wanahabari. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishna wa Polisi, Afande Isaya Mngulu, na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Bw. Richard Kayombo


ALLIANCE ONE ON TARGET FOR 2014 TOBACCO BUYING SEASON


ALLIANCE ONE ON TARGET FOR 2014 TOBACCO BUYING SEASON
The tobacco buying season which began in Tanzania during May 2014, resulted in Alliance One Tobacco Tanzania Limited (AOTTL) purchasing 28 million kgs of Flue Cured Tobacco by third week of August 2014. 
The Flue cured tobacco (FCV) was valued at 61.7million USD (Tshs 101.805 Billion) at an average price of 2.20 USD per kilo. Dark Fire cured tobacco (DFC) purchases stood at 0. 225 million Kgs valued at 0.278 million USD (Tshs 458.7 million) at an average price of 1.23 USD per kg. 
 AOTTL buys tobacco from 182 contracted Primary Societies with over 35,000 farmer members. 
 "The targets set at the beginning of the season stand at 35 million Kgs of Flue Cured Tobacco and 0.5 million kgs of Dark Fired Tobacco," said AOTTL MD Mark Mason, from Morogoro on Friday. 
"At present the bought tobacco is at 80% of the target for FCV. I am happy to report that analyzing the current buying trends it is likely that the targets will be met by the end of the buying season in October 2014 and quality has been as expected," concluded Mason. 
Purchased tobacco is transported to Alliance One factory in Morogoro for processing and selling to domestic and export customers. Purchases amounting to 15.177 million kgs of tobacco have already been received at the factory. 
The processing stage for the tobacco began in June 2014, and is scheduled to go up to December 2014. AOTTL's 50 Million USD factory employs 300 permanent staff and provides jobs for over 2000 seasonal employees at the peak of the season. 
 Tanzania Tobacco Board (TTB), the regulatory authority of the Tobacco industry in Tanzania, estimates total production in the country this season to be 104 million kgs of Flue cured tobacco valued at 219 million USD (Tshs 362 Billion) at an estimated average price of USD 2.11 per kg and 1.074 million kgs of Dark Fired Tobacco valued at 1.6 million USD (Tshs 2.640 Billion) at an average price of 1.48 USD per kg. 
Tobacco is the leading foreign exchange earner among Tanzania's traditional export crops earning the Country more than 300 million USD annually. 
Alliance One Tobacco Tanzania Ltd (AOTTL) with its headquarters in Morogoro municipality at Kingolwira township is a subsidiary company of Alliance One International (AOI) of the USA, with its headquarters in North Carolina.
 It is one of the three tobacco buying companies in Tanzania buying more than 35 million kgs of tobacco from 182 Primary Cooperative Societies with more than 39,800 farmers in Tabora, Urambo, Kahama, Manyoni, Iringa, Kasulu, Songea and Mara.
AOTTL Managing Director Mr.  Mark Mason
Part of the 28 million kgs of Flue Cured Tobacco in Mororogo


Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e- Government na ujumbe wake wamtembelea balozi wetu mdogo Dubai


Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e- Government na ujumbe wake wamtembelea balozi wetu mdogo Dubai
 Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akisalimiana  na  Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e-Government pamoja na ujumbe wake wakitokea New Delhi ambako walikuwa na mkutano na Wakala wenzao wa Serikali ya India.Katika mazungumzo yao, wamezungumzia jinsi ya kupata ufadhili kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wakala wa Serikali kwa njia ya Mtandao(e- Government)
 Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akiongea  na  Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e-Government pamoja na ujumbe wake 
 Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai akipata picha ya kumbukumbu  na  Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa e-Government pamoja na ujumbe wake 


RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAJUMBE KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA (TCD) IKULU NDOGO DODOMA LEO



RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAJUMBE KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA (TCD) IKULU NDOGO DODOMA LEO
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo akiongea na Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. ABdulrahman Kinana na Mhe Isack Cheyo walipowasili Ikulu ndogo mjini Dodoma kukutana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo. Nyuma yao ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mwenyekiti wa UPDP Mhe Fahmi Dovutwa leo.TCD inaundwa na vyama vyenye uwakilishi bungeni, ambavyo ni CCM, CUF, CHADEMA, TLP, NCCR-Mageuzi na UDP.
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) Mhe John Cheyo , Makamu Mwenyekiti wa TCD Mhe Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana, Isack Cheyo, Mhe Augustine Lyatonga Mrema na Mhe Fahmi Dovutwa wakielekea chumba cha mikutano Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo 
Wajumbe  wa TCD wakielekea chumba cha Mikutano
Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI Mhe Joseph Mbatia, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt Wilbroad Slaa wakiwasili Ikulu Ndogo mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na wakiwasili Ikulu ndogo mjini Dodoma leo
Wajumbe wa TCD wakielekea chumba cha Mikutano Ikulu ndogo mjini Dodoma leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana  na wajumbe wengine wa TCD alipokutana nao leo Ikulu Ndogo mjini Dodoma 
 Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
  Rais Kikwete akizungumza  na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania alipokutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiagana na wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
 Rais Kikwete akiagana nna wajumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania baada ya kukutana nao Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo
Rais Kikwete akiagana na mjumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania na Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustune Lyatonga Mrema Ikulu Ndogo Mjini Dodoma leo. PICHA NA IKULU