Saturday, May 31, 2014

MWENYEKITI WA WAZAZI/CCM TAIFA NA MJUMBE WA KAMATI KUU CCM TAIFA ALIPOWASILI MTWARA LEO AKITOKEA LINDI KUANZA ZIARA YA KIKAZI LIVE!!


MWENYEKITI WA WAZAZI/CCM TAIFA NA MJUMBE WA KAMATI KUU CCM TAIFA ALIPOWASILI MTWARA LEO AKITOKEA LINDI KUANZA ZIARA YA KIKAZI LIVE!!
Mwenyekiti Bulembo akivalishwa Skafu na Chipukizi.





Mwanachama mpya kutokea CUF aliporudisha kadi yake rasmi kwa Mwenyekiti Bulembo.




PRESIDENT KIKWETE SENDS CONGRATULATORY MESSAGE TO NEW MALAWI PRESIDENT




PRESIDENT KIKWETE SENDS CONGRATULATORY MESSAGE TO NEW MALAWI PRESIDENT
H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Peter Mutharika President of the Republic of Malawi. 
 The message reads as follows;

"H.E. Peter Mutharika,
 President of the Republic of Malawi,
 Lilongwe,
         MALAWI.

           Your Excellency,
I have received with great pleasure, the news of your election as the new President of the Republic of Malawi following the general elections held on 20th May 2014. I would like, on behalf of the People and Government of the United Republic of Tanzania and on my own behalf, to extend to Your Excellency, our sincere congratulations on your impressive victory and that of your Party, the Democratic Progressive Party. 
 Your victory in these heavily contested elections is a clear testimony of the trust and confidence that the people of Malawi have bestowed on you and your exemplary leadership.
 I wish you every success as you take up the responsibilities and challenges of the leadership of your great nation. It is my hope that during your tenure of office, the people of Malawi will enjoy greater prosperity and development. It is equally my hope that under your able leadership, the excellent bilateral relations existing between our countries and their people will be strengthened further and taken to even higher heights.
I look forward to working closely with Your Excellency not only in fostering our bilateral relations but also to concert our efforts in the cause for peace and stability in our region and the African Continent as a whole. 
 Please accept, Your Excellency, my best wishes for your personal good health and peace and prosperity for the people of Malawi. 

 Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

 ISSUED BY THE MINISTRY OF FOREIGN 
AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM. 

31STMAY, 2014.


Ajabu na kweli: Baba na Binti waendesha ndege ya abiria ya Kenya Airways pamoja



ajabu na kweli: baba na binti waendesha ndege ya abiria ya Kenya Airways pamoja
Captain Mwangi na binti yake wakiendesha ndege ya Kenya Airways pamoja


DKT. BILAL AHANI MSIBA WA BABA YAKE ROSTAM AZIZI JIJINI DAR LEO



DKT. BILAL AHANI MSIBA WA BABA YAKE ROSTAM AZIZI JIJINI DAR LEO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rostam Azizi, wakati alipofika nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Mei 31, 2014 kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na Baba yake mzazi aliyefariki katikati ya wiki hii. 
 
 - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waombolezaji waliofika  nyumbani kwa Rostam Azizi, Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Mei 31, 2014 kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na Baba yake mzazi aliyefariki katikati ya wiki hii.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, akitoa mawaidha wakati wa dua maalum iliyofanyika nyumbani kwa Rostam Azizi Oysterbay kumuombea Baba mzazi wa Rostam, aliyefariki katikati ya wiki hii.
 Baadhi ya waombolezaji walioshiriki dua hiyo maalum nyumbani kwa Rostam Azizi. Picha na OMR



WAMACHINGA WANAOFANYA KAZI ZAO KWENYE VITUO VYA DALADALA NA MABASI DODOMA KUONDOLEWA




WAMACHINGA WANAOFANYA KAZI ZAO KWENYE VITUO VYA DALADALA NA MABASI DODOMA KUONDOLEWA
 Kamanda wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma SSP Peter Sima akifafanua jambo  alipokuwa akizungumza na madiwani wa manispaa ya Dodoma  mwishoni mwa wiki hii.
 Meya wa Manispaa ya Dodoma Emanuel Mwiliko akifafanua jambo kwenye baraza la madiwani lililokutana mwisho wa wiki kujadili juu ya makusanyo mbalimbali ili kukamili makadilio ya mwaka huu wa fedha, kushoto ni Naibu Meya Jumanne Ngede.

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Robert Kitimbo akielezea jambo katikakikao cha baraza la madiwani  alipokuwa akiwataarifu kukabidhi ofisi ambako atakufanya julai 7 mwaka huu baada ya kustaafu, waliokaa ni Meya wa manispaa hiyo Emanuel Mwiliko, Naibu Meya Jumanne Ngede na
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Dkt David Malole.
Madiwani wa Manispaa wa Dodoma wakiwa katika ukumbi wa manispaa wakifuatilia jambo wakatiwalipokuwa kwenye baraza la kawaida la kujadili makusanyo ya mwaka wa fedha kwa kiasi walichofikisha mpaka hivi sasa ambapo zimebaki siku chache ili kuyawakilisha serekali kuu.

Na John Banda, Dodoma
IMEELEZWA kuwa kitendo cha wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) kuzagaa sehemu za watembea kwa miguu katika maeneo ya stendi ni hatari inayoweza kuwasababishia ajali wakati wowote.
Kauri hiyo ilitolewa na Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Dodoma SSP Peter Sima kwenye baraza la madiwani lilifanyika jana.
Sima alisema machinga hao ambao huuza bidhaa mbalimbali zikiwemo za masokoni katika sehemu hizo za watembea kwa miguu wakati wowote wanaweza kusababisha ajali kutokana na watembea kwa miguu kushindwa kupita na badala yake huwalazimu kupita kwenye barabara.
Alivitaja vituo hivyo kuwa ni kile cha Daladala jamatini, stendi ya mkoa (oil com) naya magali ya vijijini ya Mshikamano ambako wamachinga hao huzagaa bila hata kujali usalama wao.
Aidha aliwataka manispaa kuhakikisha wanawaelekeza machinga hao pakufanyia biashara zao lakini badala ya kuwaacha katika maeneo hayo ambayo ni hatari kwa maisha yao.
''Mhe. Meya hakikisheni wamachinga hao wanaondoka katika maeneo hayo kwa ajili ya usalama wao na kuuwema mji safi wenye muonekano wa kuwa jiji la sivyo tutawaondoa kwa nguvu kutokana na sheria
zinavyotuelekeza'', alisema Sima
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kati ya machinga hao ambao wengi wao hukimbia masokoni wakijazana kwenye vituo hivyo bila utaratibu na watendaji wa manispaa ambao wanaonekana kuwashindwa maana wamekuwa wakiachwa kuzagaa hovyo huko wakichafua madhingira katika maeneo hayo
bila kuchukuliwa hatua yoyote.



TANAPA YAWATUNUKU VYETI WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI WAANDAMIZI WALIOSHIRIKI KONGAMANO JIJINI MWANZA


TANAPA YAWATUNUKU VYETI WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI WAANDAMIZI WALIOSHIRIKI KONGAMANO JIJINI MWANZA
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi Cheti ,Mwandishi mwandamizi wa Gazeti la Raia Mwema na RAIA Tanzania kanda ya kaskazini Paul Sarwat ,Cheti hicho ni cha ushiriki wa kongamano la Wahariri wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwemo waandishi wa habari waandamizi  lililofanyika jijini Mwanza na kuandaliwa na TANAPA.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi Cheti ,Mwandishi mwandamizi wa Gazeti la The East African Adam Ihucha ,Cheti hicho ni cha ushiriki wa kongamano la Wahariri wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwemo waandishi wa habari waandamizi  lililofanyika jijini Mwanza na kuandaliwa na TANAPA.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi Cheti ,Mhariri wa Gazeti la Nipashe Beatrice Bandawe,Cheti hicho ni cha ushiriki wa kongamano la Wahariri wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwemo waandishi wa habari waandamizi  lililofanyika jijini Mwanza na kuandaliwa na TANAPA.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi Cheti ,Mhariri wa habari  Gazeti la Jamhuri Christopher Gamaina ,Cheti hicho ni cha ushiriki wa kongamano la Wahariri wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwemo waandishi wa habari waandamizi  lililofanyika jijini Mwanza na kuandaliwa na TANAPA.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa,Tanzania(TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi Cheti ,Mwandishi mwandamizi wa Gazeti la Raia Tanzania ,Claud Gwandu  ,Cheti hicho ni cha ushiriki wa kongamano la Wahariri wa habari toka vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwemo waandishi wa habari waandamizi  lililofanyika jijini Mwanza na kuandaliwa na TANAPA. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


WAZIRI WA MAMBO YA NJE UTURUKI AKUTANA NA RAIS DKT SHEIN LEO



WAZIRI WA MAMBO YA NJE UTURUKI AKUTANA NA RAIS DKT SHEIN LEO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi wa Uturuki Mhe,Ahmet Davutoglu alipofika Ikulu Mjini Zanzibar le akiwa na Ujumbe aliofuatana nao.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]


MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI TAREHE 0 1- 05 JUNI, 2014, KUFANYIKA KITAIFA MKOANI MWANZA.


MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI TAREHE 0 1- 05 JUNI, 2014, KUFANYIKA KITAIFA MKOANI MWANZA.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza
Mhe. Ernest Ndikilo akiongea na wanahabari 
Mkuu wa Mkoa wa Mwaza anapenda kuwafahamisha ya kwamba, siku ya madhimisho ya mazingira Duniani, hufanyika kuanzia  tarehe 01 hadi 05 ya mwezi Juni, kwa  kila Mwaka. Kwa mwaka 2014 shirika la Umoja wa mataifa linalo shughulikia mazingira limetangaza  Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kuwa ni "RAISE YOUR VOICE BUT NOT THE SEAL  LEVEL" kwa tafsiri ni "CHUKUA HATUA KUKABILIANA NA TABIANCHI na kitaifa" TUNZA MAZINGIRA ILI KUKABILIANA NA MBADILIKO YA TABIANCHI.

Kwa mwaka huu wa 2014 Mkoa wetu wa  Mwanza umeteuliwa kuwa mwenyeji wa kitaifa, kwa  wiki ya maadhimisho ya Mazingira Duniani, ambapo katika juma hilo shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali, kuhamasisha wananchi kuhusu utunzaji wa Mazingira  kwa njia ya Makongamano, kupanda miti, kuzoa takataka, maonesho ya utunzaji na mazingira, kuondoa magugu katika Ziwa Victoria na ufugaji wa nyuki pamoja na kufanya ziara kwenye maeneo tofauti yanayo jishughulisha na utunzaji wa mazingira ikiwemo viwanda.
 Ufungunguzi wa maadhimisho kitaifa utafanyika tarehe 02 Juni, 2014 kuanzia saa 1.00 asubuhi katika Viwanja vya Furahisha na siku ya kilele itakuwa tarehe 05 Juni, 2014 ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
 Shughuli zitakazo fanyika siku hiyo ni pamoja na-; kukabidhi vyeti kwa wadau mbali mbali wa mazingira, zawadi na tuzo za utunzaji uhifadhi wa mazingira pamoja na zawadi kwa washindi wa wa kuhifadhi mazingira.
 Aidha  Mkoa unategemea kupokea Wageni wa Kitaifa na  Kimataifa, Aidha Viongozi wa Kitaifa watatembelea Makampuni na kuona utunzaji wa Mazingira na jinsi ya kutenga taka ngumu na zisizo ngumu.
 Nichukue fursa hii kutoa rai kwenu kuwa " ukitaka kuona mgeni anafurahia makaribisho yako ukarimu ni kitu muhimu sana, Nawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kuwalaki wageni wote watakao tufikia katika juma zima hilo lakini pia kama ilivyo desturi yetu wanamwanza tuonyeshe ukarimu kwa wageni wetu na pindi waondokapo basi waikumbuke Mwanza.

"TUNZA MAZINGIRA, KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI"
IMETOLEWA NA MKUU 
WA MKOA WA MWANZA.


Wafanyakazi wa Benki ya NBC waipiga jeki timu ya watoto wenye ulemavu wa akili Zanzibar




Wafanyakazi wa Benki ya NBC waipiga jeki timu ya watoto wenye ulemavu wa akili Zanzibar
 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akipokea  msaada wa sh milioni mbili kutoka kwa Meneja wa NBC tawi la Zanzibar, Rajab Maalim (kushoto) zilizochangwa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya timu ya watoto wenye  ulemavu wa akili watakaoshiriki michezo ya olimpiki maalumu inayotarajiwa kuanza Juni 6 mwaka huu Wilayani Kibaha katika Mkoa wa Pwani. makabidhiano yalifanyika kwenye ofisi za makamu wa rais, Vuga, Zanzibar jana
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, : Balozi Seif Ali Idd akikabidhi fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa NBC nchini pamoja na yeye mwenyewe kwa  Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Olimpiki Zanzibar, Saada Hamad katika hafla hiyo mjini Zanzibar.
Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa akili watakaoshiriki michuano hiyo  wakiwa katika hafla hiyo.


Maskini:Mtoto Aliyekuwa Amefichwa Ndani ya Boksi kwa Miaka 4 Aanza Kupumulia Mashine



Maskini:Mtoto Aliyekuwa Amefichwa Ndani ya Boksi kwa Miaka 4 Aanza Kupumulia Mashine
MTOTO Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka minne mkoani Morogoro, sasa anaopumulia mashine  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Nasra, alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipohamishiwa Mei 26 mwaka huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi akitokea katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Watoto, David Kombo, aliyekuwa zamu alisema Nasra, aliwekewa mashine maalum ili kusaidia kupata hewa ya Oksijeni baada ya kuanza kupumua kwa shida.

Alibainisha kuwa hali ya mtoto huyo ilikuwa ikiendelea vizuri lakini juzi usiku ilibadilika na hivyo kuwekewa mashine ya kupumulia.

Dk. Kombo alisema kutokana na hali hiyo, madaktari wa zamu juzi waliamua kumfanyia vipimo na kubaini anasumbuliwa na Ugonjwa wa Nemonia.

Dk. Kombo, alisema mtoto huyo akipata nafuu ya ugonjwa wa Nemonia, ataendelea na vipimo vikubwa vya mwili mzima ikiwamo moyo na figo.

Alisema licha ya ya kumpatia dawa za Nemonia, wanaendelea kumpatia chakula na dawa baada ya vipimo vya awali kubaini ana Utapiamlo.

Ofisa Muuguzi wa zamu, Iluminata Sokani, alisema licha ya kupumulia mashine hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika kila wanapomfanyia vipimo kujua maendeleo yake.

Naye mama mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla ya mtoto hajawekewa mashine ya kumsaidia kupumua, alimuambia anaumia kifuani na kiunoni

Mtoto Nasra alifichuliwa na Mei 2, mwaka huu na majirani ambao walimweleza Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Dia Zongo kuwa alikuwa amefichwa katika boksi na Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Mariamu Said mkazi wa Kata hiyo mkoani Morogoro.

Majirani hao walimweleza Zongo kuwa Nasra alifichwa ndani ya boksi tangu akiwa na umri wa miezi tisa 2009 na kwamba hafanyiwi usafi wala kumtoa nje.


President Kikwete meets President of the World Bank Dr.Jim Yong kim



President Kikwete meets President of the World Bank Dr.Jim Yong kim
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets President of the World Bank Group Dr. Jim Yong Kim in Toronto Canada. Photo by Freddy Maro


Maalim Seif akabidhi kompyuta kwa Jumuiya Al-Noor Charitable Agency



Maalim Seif akabidhi kompyuta kwa Jumuiya Al-Noor Charitable Agency
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi kompyuta kwa Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya Al-Noor Charitable Agency, Sheikh Nadir Mahfoudh kwa ajili ya Radio Al-Noor ilipata ajali ya kuungua moto mwezi April mwaka huu.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi kompyuta kwa Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya Al-Noor Charitable Agency, Sheikh Nadir Mahfoudh nyumbani kwake Mbweni, kwa ajili ya Radio Al-Noor iliyopata ajali ya kuungua moto mwezi April mwaka huu. Wengine ni baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo. (Picha na Salmin Said, OMKR)


Bunge lapitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka 2014/2015



Bunge lapitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka 2014/2015
 Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda kushoto akiwa amempa mkono Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe Stephen Masele wakati akimpongeza mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka 2014/2015.
 Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda katikati akiwa akiwa ameshikana mikono  na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw.Eliakim Maswi na  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe Stephen Masele wakati akiwapongeza mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka 2014/2015.
 Waziri wa zamani wa nishati na Madini Mhe.William Ngeleja kulia akimpongeza Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw.Eliakim Maswi 
 Waziri Mkuu Mhe.Mizengo Pinda  katikati akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Prof.Sospeter Muhongo mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka 2014/2015.
  Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw.Eliakim Maswi akitoka katia ukumbi wa Bunge akiwa ameongozana na baadhi ya wabunge kutoka kushoto,Mhe.Mustafa Mkullo,Lucy Mayenga,Mhe.Rdhiwani Kikwete na Mh.Abuu Jumaa mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka 2014/2015.
Na Deusdedit Moshi  Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati.


Profesa Peter Mutharika Rais ashinda kinyang'anyiro cha Urais Malawi


Profesa Peter Mutharika Rais ashinda kinyang'anyiro cha Urais Malawi
Profesa Peter Muthirika anayeongoza chama 
cha DPP ndiye rais mteule nchini Malawi

Hatimaye Malawi imepata Rais mpya baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima. Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ni lazima ipate kiongozi wake na kuwaomba wananchi kuwa na utulivu .
                                         
Awali Jaji Kenyata Nyirenda wa mahakama kuu mjini humo jana usiku alitoa uamuzi kuwa hawezi kuvunja sheria kwa kuruhusu tume iongeze muda wa kuhesabu upya kura kwenye maeneo yenye utata.
Na kwamba sheria inaitaka tume kutangaza matokeo ndani ya siku nane na si vinginevyo. Uchaguzi wa Malawi ulifanyika Mei 20 nchini kote lakini siku moja tu baada ya kupiga kura, malalamiko yakiambatana na mapingamizi ya kisheria yakatawala kwenye mahakama kuu za Lilongwe na Blantyre.


IN LOVING MEMORY OF PROF. HELEN. I.LUGINA




IN LOVING MEMORY OF PROF. HELEN. I.LUGINA
Three painful years have already gone by since the day you answered the Lord's call on that fateful day of 31st May, 2011. Yet it feels like yesterday.

Ever since you have passed away life hasn't been the same, but by God's grace we survived the 3 years of agonizing loneliness and emptiness. Our thoughts and love for you will dwell in our hearts forever .We are still fulfilling God's will and purpose on earth until the day when God decides that we join you in the everlasting life that our Lord has prepared for his people.

You're fondly missed by your husband, children, grandchildren, in- laws, friends and relatives.
There will be a memorial mass on Saturday, May 31st, 2014 at St Joseph Cathedral at 12.45 am. Also there will be another mass on the following day on June 1st, 2014 on the second and third mass. You are all warmly welcomed.

MAY THE ALMIGHT GOD CONTINUE TO REST YOUR SOUL IN ETERNAL PEACE


President Kikwete, Canadian Prime Minister Stephen Harper and Ban Ki Moon hold a Joint Press Conference in canada




President Kikwete, Canadian Prime Minister Stephen Harper and Ban Ki Moon hold a Joint Press Conference in canada
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a closing joint press conference at the end of Summit on Maternal, Newborn and Child Health held at Fairmont Royal York hotel in Toronto, Canada, this morning. Centre is the Summit Co-Chair and host Canadian Prime Minister Right Honorable Stephen Harper and right is U.N. Secretary General Ban ki Moon.Photo by Freddy Maro.


NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU 2014-2015 CHUO CHA UALIMU RENGEMBA MAFINGA IRINGA


NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU 2014-2015 CHUO CHA UALIMU RENGEMBA MAFINGA IRINGA
USAJILI NA.TLF/011P
NAMBA YA KITUO CHA MITIHANI E.643.

CHUO KINATANGAZA NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2014 - 2015
 
NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NA CHILD DEVELOPMENT - 2014-2015
ADA YA MWAKA MOJA PAMOJA NA HOSTEL NI MILLIONI MOJA (1,000,000) UNAWEZA KULIPA KWA AWAMU NNE NDANI YA MWAKA MMOJA.
 
FORM ZA SHULE ZINAPATIKANA
 
kwa maelezo zaidi wasiliana na njia ya barua pepee; rugemba@gmail.com
 
REGEMBA CHUONI -0753 038336
DAR ES SALAAM -BOKO MAGENGENI - 0657879068 DEBORA SECRETARY
DAR ES SALAAM - BUGURUNI HOSPITAL - 0763818244 - GREENA
DAR ES SALAAM - ALMASHAURI YA TEMEKE WIZARA YA ELIMU - 0717006887 - ANNA ALPHONSO
DAR ES SALAAM-0715379940 NATALIE- MNAWEZA KUKUTANA TOWN -
 
1.MAFUNZO YA UALIMU STASHAHADA (SECONDARY) "DIPLOMA IN SECONDARY" (DSEE) KWA MIAKA 2.
sifa za muombaji awe amemaliza kidato cha sita (VI) na ufaulu wa principal (1) na subsidiary 91)
2. UALIMU DARAJA LA 111A - NGAZI YA CHETI (GATCE) KWA MIAKA 2
sifa za mwombaji: awe amemaliza kidato cha nne (1V) na ufaulu wa alama 26-27 (kwa mwaka 2004-2012)au alama 32-34 (kwa mwaka 2013)
3. MAFUNZO YA UALIMU WA AWALI (ECDE) - KWA MWAKA 1.
sifa za mwombaji; awe amemaliza kidato cha nne na ufaullu daraja 1V ya alama 42.
 
NB: Wanafunzi wote watakakosomea mafunzo ya elimu ya awali; chuo kitawapa nafasi ya kurudia mitiani ya kidato cha nne ili waweze kwenda ngazi nyingine ya juu.
 
4. MAFUNZO YA QUALIFYING TEST (QT) MIAKA 2 YANATOLEWA CHUONI
5. CHUO PIA KINATOA MAFUNZO YA KURUDIA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (kwa wale wote wanaohitaji)
 
KOZI ZINAZOTOLEWA CHUONI:
 
6. DIPLOMA IN SECONDARY EDUCATION (DSE)
kidato cha sita awe na pirncipal pass moja na subsidiary moja kwenye masomo ya kufundishia matokeo ya zamani na principal pass mbili kwa matokeo ya form six yatakayotoka mwezi wa saba mwaka huu.
7. CERTIFICATE IN EARLY CHILDHOOD DEVELOPMENT EDUCATION (ECDE)
8.DIPLOMA IN PRIMARY EDUCATION (DPE)
awe amehitimu mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi ngazi ya cheti
9. DIPLOMA IN EARLY CHILDHOOD DEVELOPMENT EDUCATION (DECDE)
sifa za muombaji; awe amehitimu mafunzo ya ualimlu wa awali ngazi ya cheti
 
10. GRADE 111A TEACHERS CERTIFICATE (GATCE)
ni elimu ya kidato cha 1V mwisho ni dividion 1V point 34 matokeo ya sasa na 27 matokeo ya zamani awe na D za BG, ENG, KISW, na MATH.