Saturday, October 25, 2014

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA MEJA JENERALI HERMAN LUPOGO



RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KATIKA MAZISHI YA MEJA JENERALI HERMAN LUPOGO
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe wakiwasili katika viwanja vya makaburi ya Kinondoni wakati wa mazishi ya Meja Jenerali mstaafu, Herman Lupogo. Meja Lupogo alifariki Oktoba 19 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo  jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa  akisalimiana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi.
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na akizungumza na Waziri wa Ulinzi wa zamani, Prof. Philemon Sarungi.
 Askari akiwa amebeba shada la maua.
 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiwasili.
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi.
 Mkuu wa Majeshi mstaafu, Robert Mboma (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiweka shada la maua.
 Mwili wa marehemu Meja Jenerali, Herman Lupogo ukiwasili makaburini.
 Gwaride likiwa mguu sawa.
 Maofisa wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Meja Jenerali Herman Lupogo.
 Maofisa wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Meja Jenerali Herman Lupogo. 
 Brass Band ikiongoza.
 Maofisa wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Meja Jenerali Herman Lupogo.
 Maofisa wa JWTZ wakiweka jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Meja Jenerali Herman Lupogo kaburini.
 Mwili ukiwekwa kaburini.
 Mke wa marehemu Meja Jenerali Herma lupogo akiweka udongo katika kaburi.
 Ndugu na jamaa wwakiweka udongo.
 Rais mstaafu, Benjamin Mkapa akiweka udongo.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi akiweka udongo.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa zamani, Edgar Maokola Majogo akiweka udongo.
Kazi ya kuweka zege katika kaburi ikiendelea.
 Mke wa marehemu akiweka shada la maua.
 Familia ikiweka shada la maua.
 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe wakiweka shada la maua katika kaburi la Meja Jenerali mstaafu, Herman Lupogo wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Meja Lupogo alifariki Oktoba 19 katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo. 
 Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akiweka shada la maua.
 Mashada ya maua yakiwekwa.
 Heshima kwa marehemu Meja Jenerali Herman Lupogo.
  Heshima kwa marehemu Meja Jenerali Herman Lupogo.
 Mwakilishi wa Jeshi,  Meja Jenerali Gaudence Milanzi akisoma wasifu wa marehemu.
 Kaburi la Meja Jenerali Herman Lupogo.
Rais mstaafu Benjamin mkapa akiagana na mke wa marehemu.

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin  Mkapa amewaongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Meja Jenerali Herman Corneli Lupogo kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine walioudhulia mazishi hayo ni, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, Jenerali Mstaafu Robert Mboma pamoja na Mawaziri waliowai kuongoza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga, Prof, Philemoni Sarungi na Edgar Maokola Majogo.

Akisoma risala mara baada ya mazishi, Mwakilishi wa Jeshi,  Meja Jenerali Gaudence Milanzi alisema, marehemu alifariki dunia mnamo Oktoba 19, mwaka huu kwa ugonjwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo alikokuwa akipata matibabu.

Alisema, marehemu alimaliza elimu ya Kidato cha sita katika shule ya Sekondari Pugu mwaka 1956, baadae akapata Stashahada ya Ualimu na Shahada ya kwanza ya Sanaa katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda.

"Marehemu alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania mnamo Julai 23, 1965 na kutunukiwa Kamisheni Januari 21, 1966 na baadae kwa nyakati tofauti alipandishwa vyeo hadi kufikia Cheo cha Meja Jenerali mnamo Februari 9, 1983 ambacho alistaafu nacho Jeshini,"alisema.

Aliongeza kuwa, baada ya marehemu kustaafu aliendelea na shughuli mbalimbali za kujenga taifa ikiwamo, kuwa Mkuu wa Mkoa Iringa mwaka 1990, Mwenyekiti Chuo cha Diplomasia 1987 hadi 1991, Mkurugenzi Mtendaji wa AICC 1993.

"Pia alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS), 2001 hadi 2014, marehemu mara kwa mara alienda kushiriki kutoa mihadhara kama mwalimu wa kualikwa katika Vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya Jeshi ikiwamo Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC),"alisema.

Aidha, alimalizia kwa kutoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma wa JWTZ kutokana na msiba mzito uliotokea na kwamba sio pigo kwa familia yake, bali kwa ndugu, jamaa, majirani, jeshi na Taifa kwa ujumla.