Saturday, September 13, 2014

Wateja 225,000 wa Vodacom wajiunga na huduma ya ujumbe mfupi ya uzazi salama



Wateja 225,000 wa Vodacom wajiunga na huduma ya ujumbe mfupi ya uzazi salama
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid (kushoto) akimsikiliza Ofisa Mkuu wa taasisi ya Udhibiti na Kinga ya Magonjwa ya CDC, Angela Makota (kulia) kwenye makabidhiano ya hundi ya Sh. Milioni 149 iliyotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuboresha huduma ya afya na Uzazi na Mtoto inayojulikana kama Wazazi Nipendeni.Makabidhiano yalifanyika katika ofisi ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam jana.Katikati ni Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagaghywa.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Waziri wa Afya (kushoto) akipokea mfano wa hundi wa fedha Sh.Milioni 149 iliyotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuboresha huduma ya afya na Uzazi na Mtoto inayojulikana kama Wazazi Nipendeni. Anayekabidhi ni Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusuiano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mutagaghwa.Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya wizara hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Mkuu wa taasisi ya Udhibiti na Kinga ya Magonjwa ya CDC, Angela Makota.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid (katika) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, kituo cha Udhibiti na Kinga cha CDC na wizara hiyo mara baada ya makabidhiano mfano wa hundi ya fedha Sh.Milioni 149 iliyotolewa na Vodacom Foundation kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya kuboresha huduma ya afya na Uzazi na Mtoto inayojulikana kama Wazazi Nipendeni. Hafla ya makabidhiano yalifanyika katika ofisi za wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam jana.