Monday, June 09, 2014

Papa awapokea Peres na Abbas



Papa awapokea Peres na Abbas
Mahmoud Abbas, Papa na Shimon                Peres Vatikani
Papa Francis amewapokea viongozi wa Israil na Palestina katika Vatikani.
Rais Shimon Peres wa Israil na Mahmoud Abbas wa Palestina walikutana Vatikani kuomba amani Mashariki ya Kati.
Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya nyumba yake, kabla ya kusafiri pamoja naye na kiongozi wa kanisa la Orthodox, Askofu Mkuu Bartholomew, hadi kwenye sherehe katika bustani ya Vatikani.

Wakitarajiwa kupandisha mzaituni kama alama ya kudumu ya hamu ya pande zote mbili ya kupata amani baina ya watu wa Israil na Palestina.
Papa alisema yeye hataki kuhusika moja-kwa-moja na mazungumzo ya amani, lakini anatumai viongozi hao wakikutana, huenda ikasaidia kupunguza uhasama kati yao