Sunday, September 30, 2012

NATHAN ATOA ZAWADI KWA WATOTO WANAOUMWA UGONJWA WA SARATANI


  Mchora vibonzo, Nathan Mpangala, akitoa maelekezo ya jinsi ya kuchora vibonzo kwa baadhi ya watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbil, Jijini Dar es Salaam, Jumamosi, 29.09.2012. Ziara hiyo ni sehemu ya maadhimisho miaka sita ya KIBONZO kinachorushwa ITV na pia ni sehemu ya shughuli za kijamii ya Tuzo ya Mchora Katuni Bora wa 2011, aliyopewa na Baraza la Habari Tanzania, (MCT).
 Mchora katuni wa gazeti la Tanzania Daima, Said Michael, aliyechutama, akiwaelekeza baadhi ya watoto wanaosumbuliwa na saratani jinsi ya kuchora katuni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, jana. (29.09.2012). Said, alikuwa miongoni mwa wachoraji katuni waliungana kumsindikiza mchoraji mwenzao, Nathan Mpangala, aliyekwenda kutembelea watoto hao ili kuwapa zawadi na kuchora nao ikiwa maadhimisho miaka sita ya KIBONZO kinachorushwa ITV na pia ni sehemu ya shughuli za kijamii baada ya kupata tuzo ya uchoraji bora wa katuni, 2011 aliyopewa na Baraza la Habari Tanzania, (MCT).

Mnyama (SIMBA) wa Msimbazi aendelea kuunguruma




 Mshambuliaji wa Simba, Felix Sunzu akiwatoka mabeki wa Tanzania Prisons katika mechi ya Ligi kuu ya Vodacom nesho. Simba ilishinda 2-1
 Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kwanza lililofungwa na Felix Sunzu (kulia)
 Mashabiki wa Simba wakishangilia

TRENI YA TAZARA ITAKAYOTUMIKA KWA USAFIRI WA DAR ES SALAAM –MWAKANGA-KURASINI YAFANYIWA MAJARIBIO



 Treni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),likiwa katika stesheni ya Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya Majaribio iliyofanyika kutoka Dar es Salaam-Mwakanga-Kurasini-Dar jna mchana. Treni hiyo kwa kuelekea Mwakanga itapita  Kwa fundi Umeme, Kwa Limboa, Lumo(Kigilagila), Sigara, Kitunda, Kupunguni B, Majohe, Magnus na Mwakanga. Na kuelekea Kurasini Itatokea Dar,Kwa fundi Umeme,Yombo,Chimwaga,Maputo,Mtoni Relini,Kwa Azizi Relini na kishia Stesheni ya Kurasini.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA)na wa Wizara ya Uchukuzi wakiwa ndani ya Mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio kwa ajili ya Usafiri wa treni Jijini Dar es Salaam jana.

 Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia(TAZARA),Mhandisi Abdalla Shekimweri akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo jana wakati wa majaribio ya Mabehewa matatu yakayofanya safari zake kutokea Dar-Kurasini-Mwakanga.Mabehewa hayo ni sehemu tu ya mabehewa yatakayokuwa yakifanya safari hizo.

Meneja Mkuu wa Kanda ya Tanzania wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), Mhandisi Abdalla Shekimweri,akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (aliyevaa shati la rangi ya zambarau)katika kituo cha Mwakanga wakati wa majaribio ya mabehewa matatu ya TAZARA yatakayotumika kwa Usafiri wa Dar es Salaam jana.Mabehewa hayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 80 waliokaa kwenye Siti na yanatarajiwa kuanza kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam-Mwakanga na Dar es Salaam-Kurasini kuanzia mwezi Oktoba Mwaka huu.

Mtoto Anusurika Kifo Mabibo





 Akiwa amebebwa na mtu ambaye jina lake halikufahamika mara na iwapo ni mzazi wake,mtoto huyu amegongwa na gari na mwenye gari hakusimama.

MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI WA CCM WILAYANI RUNGWE.



PROF MARK MWANDOSYA

Uchaguzi wa ngazi mbalimbali za CCM wilayani Rungwe mkoani Mkoani Mbeya matokeo ya awali ni 

Waliogombea nafasi ya NEC Prof Mark Mwandosya amepata kula 1118 na aliemfuatia ni Richard Kazsesela kula 198 ndugu mwandiga kula 28, zilizoharibika kula 12 

Aliechaguliwa nafasi ya mkutano mkuu wa mkoa Michael Pascco, Doriss Kimambo.
 Mkutano mkuu wa Taifa walio chaguliwa ni Petro Paresso, Lutengano Mwalwiba , Richard Kasesela, Sarome Mwakalinga, Meckson Mwakipunga,

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Willbroad Slaa amepokea wanachama wapya kutoka familia ya mwanasiasa mkongwe nchini na Waziri wa Nchi 0fisi ya Rais(Mahusiano na Uratibu) Mh Stephen Wasira,Estha Wasira na Lilian Wasira.



Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, akiwakabidhi kadi ya uwanachama wa chama hicho kwa Lilian Wassira na ndugu yake Esther, baada kujiunga na chama hicho. Lilian na Esther ni watoto wa George Wassira Kaka wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano) Stephen Wassira.Picha na Michael Matemanga-Mwananchi)
-----
Baada ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache zilizopita, leo tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia virago Chama cha Baba yao CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa ni kamanda Ester Wasira na Lilian Wasira.

Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO):(i) Alielezea furaha yake kwa kujiunga na chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa Mtanzania

(ii) Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia CHADEMA kura

(iii) Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala. Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi.

(iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo.

(v) Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa. Amewapa moyo viongozi wa CHADEMA wasitishwe na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama itambidi afanye hivyo.

(vi) Kwamba CHADEMA ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura.

(vii) Naye alimalizia kwa kusema, “Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja.” Dkt. Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C.

Ligi kuu ya Vodacom sasa mambo safi.



·        Sintofahamu kati ya TFF na Klabu zafikia mwisho.
·         Vodacom yatoa fedha na Vifaa kwa timu zinazoshiriki ligi kuu.
·         Yaahidi makubwa zaidi.

Dar es Salaam, 30 Septemba, 2012.

 Kufuatia kukaa katika kikao cha majadiliano kati ya Mdhamini mkuu wa ligi kuu Vodacom Tanzania, kamati ya ligi, TFF na vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo, Mashabiki na wapenzi wa soka nchini wameondolewa hofu juu ya udhamini wa ligi inayoendelea hivi sasa.

Mdhamini mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania, imekubali kuendelea kuunga mkono ligi hiyo na kuwaomba mashabiki wa soka kutegemea msimu mzuri wa ligi mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, amesema kuwa mvutano ambao umekuwepo baina ya baadhi ya Vilabu vya soka na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na wadhamini sasa yamepatiwa ufumbuzi.

“Kulikuwa na sinto fahamu kati ya Klabu za ligi kuu TFF na sisi kama wadhamini, tulikaa kikao siku ya ijumaa na wadau wote wa ligi na sasa mambo yote yamewekwa katika msitari,” alisema Kelvin na kuongeza kuwa “ Tumedhamiria kuendelea kuiunga mkono Ligi kuu ya Vodacom hatukuwa na matatizo yoyote katika kusaini mkataba na kamati ya ligi ni ufafanuzi tu ndio ulihitajika  ili kuwekana sawa,” alisema Twissa.

Kuhusiana na kutolewa kwa fedha za udhamini na uendeshaji wa ligi na udhamini wa kampuni pinzania twissa alisema Vodacom haizuii klabu za ligi kudhaminiwa na kampuni nyingine yoyote tofauti na zile zenye msingi wa kiushindani katika biashara na kampuni hiyo.

“Kufuatia kikao hicho na kuwa katika msitari mmoja tumekwisha toa fedha na vifaa kwa TFF na vilabu ili ligi iweze kwenda kama ilivyo takiwa,Tukiwa kama wadau katika kuunga mkono maendeleo ya soka nchini, tumeruhusu kampuni nyingine ambazo hazina upinzani wa kibiashara na sisi ili kuondoa muingiliano wa kimaslahi,” alisema.

“TFF inadhamana ya kusimamia sheria na masharti kuhusu ligi. Hatuna matatizo yoyote ya kiutendaji na TFF wala klabu yoyote” alihitimisha Twissa.

Ligi kuu ya Vodacom ilianza rasmi tarehe 15  mwezi septemba, na tutashuhudia michezo 182 kwa kushirikisha timu 14 zinazoshiriki katika ligi hiyo, zikiwemo Yanga Afrika, Kagera sugar, na Simba ambaye ndie bingwa mtetezi wa ligi kuu ya Vodacom.

Kampuni ya Vodacom imekuwa mdhamini wa ligi kuu kwa miaka mitano sasa, na imesaini mkataba mpya wa udhamini wa ligi hiyo kwa miaka mitatu na shirikisho la mpira wa miguu TFF, mkataba utakao shuhudia shirikisho hilo likipokea udhamini wa kila msimu kwa miaka mitatu mfululizo.

Mwisho.

CHEKA AMGALAGAZA KARAMA RAUNDI YA SITA



Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.

 Refarii wa mpambano akiwaelekeza mabondia wasicheze kwa kukumbatiana.


Bondia Fransic Cheka kushoto akipepesuka baada ya kupigwa ngumi na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K.O raundi ya sita na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa.


Bondia Fransic Cheka kushoto akimshambulia Karama Nyilawila kwa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi Cheka alishinda raundi ya sita baada ya kumpiga na kudondoka chini baada ya kuesabiwa akashindwa kuendelea.


Bondia Karama Nyilawila  kulia akijitaidi kukwepa makonde ya mpinzani wake Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita.



Mabondia Karama Nyilawila kushoto akionesheana umwamba wa kutupa masumbwi na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao cheka alishinda kwa K,O Raundi ya sita.

Fransic Cheka kushoto na Karama Nyilawila wakiwa uringoni kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi Cheka alishjnda kwa K,O ya Raundi ya sita 


Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Fransic Cheka wakionesheana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita 



Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.


Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.

Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

WAKRISTO WAKUMBUSHWA KUWA WASISUMBUKIE MAISHA BALI WAENDELEE KUMNGOJA YESU ATAWAJAZA.



 Wakati wa kusifu na kuabudu katika kanisa la EAGT City Centre kama inavyoonekana katika picha ambapo kamera yetu ililinasa tukio hili katika ibada ya jumapili ya leo. Wapiga vyombo wa Kanisa la City Centre wakionekana wakiwa wanafanya kazi yao kama kawaida.
 Wakati wa kumsifu Mungu hakuna ambaye anaambiwa cheza hivi au fanya hivi, hapa kila mmoja anamchezea Mungu kwa jinsi Mungu alivyotenda Mambo makuuu katika maisha yake.
 Praise team kutoka kanisa la City Centre wakiimba kwa umakini sana kwa sauti nzuri ambazo Mungu amewapa.
 Hawa ni wakristo ambao wameleta Fungu la Kumi, moja kati ya hatua ya mkristo katika makuzi ya kiroho. Kama wewe ni mkristo ni wajibu wako kutoa fungu la kumi kwa yote unayopata katika biashara yako.
 Kwaya ya EAGT City Centre wakiimba wimbo mzuri sana ambapo kila mkristo aliyefika katika kanisa hilo alibarikiwa, hapa soloist Mr Paulo anaongoza kikosi kazi cha kwaya hiyo.
                      Kwa Yesu kuna raha sanaaaaa.
       Wanacheza kwa staili nzuri kama inavyoonekana.
 Wakristo wa kanisa hilo wakisikiliza neno la Mungu kwa umakini huku wakiendelea kupokea upako wa Mungu ambao si wa kawaida.
                               Kwa Mungu mambo kama haya yapooo, wala usihofu.
 Wakristo wakionekana wamejaa upako sana na huu ni upande wa kina baba kama walivyokamatwa na kamera yetu katika ibada ya Jumapili.

.Wakristo wakumbushwa jinsi Mungu alivyo mkuu.
.Waambiwa wasisumbukie maisha.

Wakristo wamekumbwa kuwa na Yesu siku zote katika maisha yao na kuendelea mbele na safari ya kwenda mbinguni kwa kuwa wanakabiliwa na mambo magumu sana katika maisha ya kila siku na hivyo kama hawatakuwa makini wanaweza wasimalize safari yao vizuri. 
Haya yamesemwa na Mtumishi wa Mungu Mama Mchungaji Amasi katika ibada ya jumapili katika kanisa la EAGT City Centre kanisa linalioongozwa na Mchungaji Michael Kulola wakati akihubiri neno la Mungu katika kusanyiko la Watu wa Mungu.
Amesema kuwa maisha ni muunganiko wa mambi mengi sana na yote yanamkabili mkristo na  kuomba kuwa makini katika kuyakabili yote yanayokuja mbele yake na kumwomba Mungu sana kila mara ili aweze kukupa ngvu katika kushinda majaribu yote amabyo shetani anayaleta katika maisha ya kila siku katika mkristo.
Ametoa mfano kuwa watu wengi wamepoteza mwelekeo wa Mungu na kushindwa kuendelea katika safari ya kwenda mbinguni kwa kuweka mbele suala la maisha mbele hivyo kupoteza kila upako wa thamani ambao mkristo ameupata wakati alipokubali kuokoka na kuwa mfuasi wa Yesu kristo.

Mambo yaliojiri leo katika Magazeti Jumapili 30/09/2012