Saturday, August 25, 2012

Magazeti Leo Jumamosi



 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MABADILIKO YA RATIBA YA UCHAGUZI WA VYAMA WANACHAMA WA TFF


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko madogo katika ratiba za uchaguzi za wanachama wa TFF. Ratiba za uchaguzi za vyama wanachama wa TFF ambavyo vimekwishaanza mchakato na ambavyo havijaanza mchakato wa uchaguzi itakuwa kama ifuatavyo:

CHAMA MWANACHAMA WA TFF
Tarehe ya Kuanza Mchakato wa uchaguzi
Tarehe ya Uchaguzi
Arusha Region Football Association (ARFA)
27-Aug-2012
7-Oct-2012
Dar es Salaam Region Football Association (DRFA)
3-Sep-2012
14-Oct-2012
Geita Region Football Association (GEREFA)
29-Sep-2012
10-Nov-2012
Iringa Region Football Association (IRFA)
28-Jul-2012
8-Sep-2012
Katavi Region Football Association
29-Sep-2012
10-Nov-2012
Kigoma Region Football Association (KRFA)
21-Jul-2012
1-Sep-2012
Kilimanjaro Region Football Association (KRFA)
31-Jul-2012
8-Sep-2012
Lindi Region Football Association (LIREFA)
8-Sep-2012
20-Oct-2012
Manyara Region Football Association (MARFA)
21-Jul-2012
15-Sep-2012
Mbeya Region Football Association (MREFA)
8-Sep-2012
21-Oct-2012
Mwanza Region Football Association (MZFA)
29-Sep-2012
8-Nov-2012
Njombe Region Football Association (NJOREFA)
4-Aug-2012
15-Sep-2012
Coast Region Football Association (COREFA)
3-Sep-2012
14-Oct-2012
Rukwa Region Football Association (RUREFA)
27-Aug-2012
7-Oct-2012
Football Association of Ruvuma (FARU)
22-Sep-2012
3-Nov-2012
Shinyanga Region Football Association (SHIREFA)
8-Sep-2012
20-Oct-2012
Simiyu Region Football Association (SIFA)
15-Sep-2012
27-Oct-2012
Tabora Region Football Association (TAREFA)
27-Aug-2012
6-Oct-2012
Tanga Region Football Association (TREFA)
22-Sep-2012
3-Nov-2012
Tanzania Football Coaches Association (TAFCA)
29-Sep-2012
10-Nov-2012
Tanzania Sports Medicine Association (TASMA)
15-Sep-2012
27-Oct-2012
Soccer Players Union of Tanzania ( SPUTANZA)
15-Sep-2012
28-Oct-2012
Football Referee’s Association of Tanzania (FRAT)
21-Aug-2012
30-Sep-2012
Tanzania Women Football Association (TWFA)
22-Sep-2012
4-Nov-2012
TFF inavitaka vyama wanachama wake kuzingatia kikamilifu ratiba hii iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF katika kutimiza wajibu wao wa kikatiba.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF haitabadilisha ratiba hiyo kutokana na wilaya yoyote kutokamilisha uchaguzi wake, na hivyo inazitaka Kamati za Uchaguzi za Mikoa kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwa mujibu wa ratiba hii.
Kamati pia inazitaka Kamati za Uchaguzi za Mikoa kusimamia kikamilifu na kwa umakini chaguzi za wilaya zinazoendelea kwenye wilaya zilizo mikoani kwao. Ni muhimu kwa kamati kuhakikisha Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF zinafuatwa na kusimamiwa kwa umakini.

Kamati ya Uchaguzi ya TFF pia imebaini kuwa kuna Kamati za Uchaguzi za Mikoa ambazo hazikusimamia kikamilifu chaguzi za viongozi wa wilaya, kitu ambacho kinaweza kusababisha matatizo hapo baadaye. Kwa mara nyingine, Kamati ya Uchaguzi ya TFF inazitaka Kamati za Uchaguzi za Mikoa kuhakikisha wanaoomba kugombea uongozi kwenye wilaya, wana sifa zinazolingana na utashi wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF na Katiba.

Wanachama ambao hawakuzingatia ratiba hiyo, hawatapewa fursa nyingine ya kubadilisha tarehe za uchaguzi na hilo litakapotokea hatua za kikanuni zitachukuliwa.

Angetile Osiah
KATIBU MKUU

Friday, August 24, 2012

Karakana Ya Wonder Yanufaika Na Vyuma Chakavu Kutoka TBL



 
Wafanyakazi wa Karakana ya Wonder wakinyanyua moja ya nembo (logo) iliyotengezwa kwa vyuma chakavu
 
Meneja Usalama wa mahali pa kazi Renatus Nyanda (kushoto) akisaidia kufunga mlango wa Pick Up baada ya kupakia vyuma chakavu vilivyokusanywa kiwandani hapo kwa ajili ya kutengenezea vifaa 
 
Fundi Mchundo (Welder), Seif Chambela akiwa na sanamu ya tembo iliyotengenzwa kwa kutumia vyuma chakavu katika Karakana ya Wonder (Wonder Workshop)Wafanyakazi wa Karakana ya Wonder (WonderWorkshop), Msasani, Dar es Salaam
 
Meneja Mradi wa Wonder Workshop, Lisette Westerhuis, akimuonesha Meneja Mawasiliano na Habari wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi, sanamu ya ndege aliyetengenezwa kwa kutumia vyuma chakavu hivi karibuni katika karakana hiyo iliyopo Msasani, Dar es Salaam. TBL itakuwa inaipatia kila mara Karakana hiyo vyuma chakavu na makasha kwa ajili yakutengenezea vifaa mbalimbali zikiwemo sanamu za wanyama.

 
Meneja Mawasiliano na Habari wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto) akiwasaidia wafanyakazi wa Karakana ya Wonder,Nico Ngalawa (kulia) na Hafidh Selemani wakipakia kwenye gari vyuma chakavu walivyopewa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), vilivyokusanywa juzi katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Ilala Mchikichini, Dar es Salaam.
 
Baadhi ya sanamu zilizotengenezwa kwa kutumia vyuma chakavu zikiwa zimepambwa katika moja ya bustani katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
 
Mfanyakazi wa Wonder Workshop akijiandaa kuchonga chupa ili kupata bilauri hivi karibuni katika karakana hiyo.



Mama Shujaa Wa Chakula Yapata Mdhamini-NMB



 
 
Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing (Kulia) akizungumza katika hafla hiyo (kutoka kushoto)ni Mkurugenzi wa Maisha Plus, Masoud Ally na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Monica Gorman.


 
 
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam, Monica Gorman (Kulia) akizungumza katika hafla hiyo, kushoto ni Mkurugenzi wa Maisha Plus, Masoud Ally.

 
 
Meneja Mawasiliano wa NMB Josephine Kulwa akifafanua jambo.


Mpango wa Mama Shujaa wa chakula unaoratibiwa na shirika la Oxfam ulianziashwa mwaka jana hapa Tanzania. Dhumuni likiwa ni kuthamini, kuwahamasisha na kuwasaidia wanawake wote katika uzalishaji wa chakula.

NMB kwa kutambua kuwa kilimo ndiyo shughuli kuu ya uchumi Tanzania na ikiwa benki yenye mtandao mpana zaidi Tanzania imetoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya kuunga mkono mpango huu wa Mama Shujaa wa chakula kupitia kipindi cha televisheni kiitwacho Maisha Plus kinakachotarajiwa kurushwa mapema Oktoba mwaka huu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bw. Mark Wiessing alisema,

udhamini huo ni sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira miongoni mwa wanawake.

“Tumeamua kudhamini mpango huu kwa lengo la kuwasaidia kinamama ambao ni wazalishaji wadogo wa mazao mbalimbali,ili waweze kupiga hatua katika kilimo kupitia mpango huu wa Mama shujaa wa chakula”alisema Mark.

Katika kuchochea maendeleo ya kilimo, NMB ni benki ya kwanza kuanzisha akaunti maalum kwa ajili ya wakulima iitwayo NMB Kilimo Account. Pia imeanzisha huduma ya mikopo kwa ajili ya mazao mengi ya kilimo ikiwemo chai,kahawa,miwa,alizeti,korosho na mazao mengine.

Mbali ya kutoa fedha na kusaidia wakulima katika maeneo mabalimbali, NMB imeongeza mikopo zaidi katika sekta ya kilimo hasa kwa wasambazaji na watengenezaji wa chakula toka mzalishaji mdogo hadi wasambazaji wakubwa.Vilevile NMB imesaidia vyama vya ushirika zaidi 600 vyenye zaidi ya wakulima 500,000 ambao ni wanachama.

NMB kupitia mpango wa NMB Finacial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha itapata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha, uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine mengi.Kama msemo wa kiswahili unavyosema” Ukimwelimisha mwanamke umeelimisha Jamii” .NMB inaamini NMB financial Fitness itamwezesha kila mwanamke kuwa na matumizi mazuri ya kifedha na kuwa na msingi mzuri wa maisha.

Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam ,Monica Gorman pamoja na Mkurugezi wa Maisha Plus kwa nyakati tofauti waliishukuru NMB kwa mchango wake wakiamini washiriki 15 wa Mama shujaa wa chakula na 15 toka Maisha plus watafaidika na mpango wa NMB Financial Fitness. Chanzo: www.fullshangweblo.com 

Magazeti Leo Ijumaa ya Tarehe 24/8/2012



 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Thursday, August 23, 2012

Hukumu Igunga Yaivuruga CCM



 

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikitangaza kusudio lake la kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, iliyotengua ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Dk. Dalali Kafumu, wadau mbalimbali wameipongeza hukumu hiyo wakiita ni darasa tosha kwa demokrasia ya mfumo wa vyama vingi.

Miongoni mwa waliosifu hukumu hiyo ni pamoja na Spika mstaafu, ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta, akisema kuwa maamuzi hayo inafaa yaheshimiwe.

Akizungumza jana mjini Tabora, Sitta alisema kuwa mahakama ina mamlaka yake kisheria, hivyo wana CCM hawana budi kuyaheshimu maamuzi hayo kwani imefanya kazi yake inavyotakiwa.

“Kama kuna mtu anaona hukumu hiyo haikutenda haki, anaweza kwenda mahakamani kukata rufaa, lakini mimi nashauri ni vema tujipange upya tuingie ulingoni.

“Hapa mimi sina maoni juu ya jambo hilo, bali cha msingi ni vema tukakaa na kutafakari yaliyotokea huko Igunga, ili basi tukiona inafaa kukata rufaa sawa, na kama tuingie ulingoni, yote ni sawa,” alisisitiza Sitta.

Katika hukumu yake juzi, Jaji Mary Nsimbo Shangali, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa CHADEMA, Joseph Kashindye, alisema kuwa alipokea malalamiko 15 ambayo yaliridhiwa na pande zote mbili, lakini yakaongezwa madai mengine mawili na kufikia 17.

Mbali na Dk. Kafumu, washitakiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Msimamizi wa uchaguzi jimboni humo, Protace Magayane na kwamba mahakama hiyo ilithibitisha madai saba ya kutengua matokeo hayo.

Hata hivyo, wakati Sitta akiwa na mtazamo huo, CCM kupitia kwa Katibu wake wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ilieleza kutoridhishwa na hukumu hiyo, hivyo kuamua kukata rufaa.

Pamoja na CCM kuchukua hatua hiyo, wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa na wanaharakati waliliambia Tanzania Daima kuwa, hukumu hiyo ni darasa tosha la demokrasia linaloonesha jinsi sheria za uchaguzi zinavyovunjwa.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashir Ali, alisema hukumu hizo za uchaguzi ikiwamo hiyo ya Igunga, zina maana sana kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya Siasa, wanasiasa na wananchi.

“Tatizo letu huwa hatusomi hukumu hizi kwa undani, kwani tungekwishajua kuwa ni darasa tosha la demokrasia. Suala la takrima lilikuwa halieleweki kama ni rushwa, ushindani wetu wa kisiasa si wa kuvumiliana, una matumizi makubwa ya fedha, mali za serikali na madaraka kwenye kampeni,” alisema.

Ali alifafanua kuwa hukumu hiyo imetoa mwanga kuwa, kama hakuna chombo huru cha kusimamia sheria zinazokiukwa ni sawa na bure, akitolea mfano Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa licha ya kuwapo wakati wa mchakato huo, vilishindwa kuchukua hatua.

“Kuna mjadala kuhusu uwepo wa sheria ya Tume ya Uchaguzi, maana tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hakuna sheria ya Tume ya Uchaguzi, badala yake chombo hiki kinatambuliwa na sheria za uchaguzi, jambo linalotoa mwanya kwa mapungufu yanayojitokeza sasa,” alisema.

Kuhusu uwajibikaji wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakati wa uchaguzi huo mdogo, Ali alisema kuwa mpaka sasa umuhimu wa ofisi hiyo hauonekani maana kama hoja ni kusajili vyama, kazi hiyo inaweza kufanywa hata mahakamani.

Alibainisha kuwa, kwa sasa ofisi ya msajili na Tume ya Uchaguzi ni kama idara tu ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo wananchi wanapaswa kutumia hukumu ya Igunga kama tathmini wakati huu wa mchakato wa katiba mpya kusahihisha makosa ya kuvifanya vyombo hivyo huru.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Bara, Mtatiro Julius, alisema hukumu hiyo itawafungua wananchi kuona umuhimu wa kubadilisha mfumo wa uchaguzi ili kuepusha taifa kuingia gharama zisizokuwa za lazima pale kiongozi anapokufa ama kuenguliwa.

“Hii naiona kama hatufikirii sawa sawa, maana matumizi ya mabilioni ya fedha kwenye uchaguzi yalikuwa kwa vyama vyote kule Igunga hasa CCM, CHADEMA na CUF. Lakini hili linaweza kuepukwa mana kama upuuzi unafanywa na watu wawili, hatuna sababu ya kulisababishia taifa hasara,” alisema.

Kwa mujibu wa Mtatiro, inapotokea hali kama hiyo ya mbunge kuenguliwa au kupoteza maisha, mshindi wa pili kutoka chama kingine ndiye achukue nafasi badala ya kurudia uchaguzi.

“Igunga tuliona Dk. Kafumu walipishana kidogo na Kashindye wa CHADEMA, hivyo kwa vile huyu alikiuka taratibu, basi mshindi wa pili apewe nafasi kuliko kurudia uchaguzi, kwani kufanya hivyo kunaweza kukipa chama kilichoenguliwa ushindi tena wa mtu asiyefaa,” alisema Mtatiro.

Mwanasiasa huyo pia hakusita kuinyoshea kidole Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, akisema kuwa, John Tendwa (msajili) ameonesha wazi ni wakala wa CCM anayefanya mbinu za kukisaidia chama hicho kishinde badala ya kusimamia kanuni na sheria.

Mtatiro aliweka bayana kuwa makosa yaliyoainishwa kwenye hukumu iliyomtia hatiani Dk. Kafumu na kumnyang’anya ubunge wake, yalilalamikiwa mapema na wapinzani kwa Msajili wa Vyama wakati wa kampeni, lakini hakuchukua hatua yoyote.

“Msajili wa vyama hana meno, na huyu amekuwa na kashfa ya kusajili hata vyama visivyo na sifa ilimradi tu aweze kuvidhoofisha vyama makini vya upinzani. Hata kwenye uchaguzi ameonesha wazi anataka CCM ishinde,” alisema.

Mtatiro aliongeza kuwa, umefika wakati nafasi hizo nyeti za vyombo kama Tume ya Uchaguzi, Msajili na nyinginezo zitangazwe ili watu wenye taaluma zao washindanishwe na kuchujwa na chombo maalumu badala ya kuteuliwa na rais.

Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Ananilea Nkya, alizungumzia hukumu hiyo ya Igunga akisema imetoa tafsiri mpya kwa wananchi kuelewa demokrasia ya vyama vingi na namna ya kumpata mwakilishi makini bila rushwa na vitisho.

“Hili litakuwa fundisho kwa wanasiasa wanaochezea fedha nyingi kwenye uchaguzi kununua watu, maana watatambua sasa kuwa kufanya hivyo kutawapotezea viti vyao. Lakini na wagombea wanapaswa kuwa makini na wapiga debe na vyama vyao, kwani wanaweza kuingizwa mtegoni kama alivyoponzwa Dk. Kafumu,” alisema.

Akisoma hoja zilizothibitishwa na mahakama hiyo juzi, Jaji Shangali alisema ni pamoja na Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kutumia nafasi yake ya uwaziri kutoa ahadi ya ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo lilikuwa ni moja ya kero kubwa kwa wananchi wa Igunga.Waziri Magufuli akiwa katika uchaguzi mdogo huo katika moja ya kampeni, alitumia nafasi ya uwaziri kuwatisha wapiga kura wa jimbo hilo kuwa kama hawatamchagua mgombea wa CCM watawekwa ndani.

Jaji Shangali pia alisema kuwa Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage, alipita mitaani akitangazia wananchi kuwa mgombea wa CHADEMA amejitoa.

Katika hoja nyingine ni kwamba Imamu Swalekh Mohamed wa Mskiti wa Ijumaa Igunga, aliwatangazia waumini wa Kiislamu kuwa wasiichague CHADEMA kwa kuwa baadhi ya viongozi wake walimdhalilisha Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario.

Nayo matamshi ya Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kudai kuwa CHADEMA imeleta makomandoo kuuvuruga uchaguzi huo ni mojawapo ya hoja ambazo mahakama hiyo ilizikubali.

Katika hoja kuu ya mahindi, Jaji Shangali alihoji kama wananchi wa Igunga walikuwa na njaa sana. Na kwamba, kama jibu ni ndiyo, ni kwanini uchaguzi usifanyike wakati hawana njaa.

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YABADILI UTARATIBU WAKUTEUA WAJUMBE WA BODI



 
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki amebadili taratibu za kuwapata wajumbe wa Bodi mbali mbali zilozoko chini ya Wizara. Kuanzia sasa Wajumbe wa Bodi hizo watapatikana kwa njia ya ushindani badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Waziri.

Kwa sasa kuna Bodi nane (8) ambazo muda wake umeisha au unakaribia kuisha.Bodi hizo ni za za Taasisis/Mashirika yafuatayo;-

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
Makumbusho ya Taifa
Chuo cha Mafunzo na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA)
Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi
Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA)
Bodi ya Leseni za Utalii (TTLB)

Watanzania wenye sifa za kuwa Wajumbe wa Bodi hizo wanatakiwa kupeleka maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Maelezo zaidi ya namna ya kupeka maombi yataweka kwenye magazeti na tovuti ya Wizara,www.mnrt.go.tz 

BBC Kutangaza Dira Ya Dunia Na Star TV


 

 

 
 Sophie West, Afisa mahusiano wa BBC
 
 Mandhari ya hotelini

 
 Kuonyesha matukio
 
 Watangazaji kazini
 
 Neville Meena Kutokea Mwananchi Communication

BBC Inazindua matangazo ya DIRA YA DUNIA programu ya Kiswahili kwa Television kupitia Star TV. Jumatatu hadi Ijumaa saa 3 usiku.Uzinduzi huu unafanyika sasa hivi Harbour View Hotel,Samora Avenue Dar

Ratiba ya Ligi Kuu ya Uingereza Wiki Hii



Dkt. Mwakyembe amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bandari

By Lokissa:



Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.

Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.

Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.

Waziri Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wadau wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na imani na watumishi wake kitu kinachoifanya serikali kukosa mapato.

Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.
 

Source:Jamii Forums