Sunday, October 24, 2010

Hii number 25570781639 ni ya wapi na TCRA wanajua hili?

Leo nimepokea SMS kutoka hiyo number juu jamaa ameandika kuwa kuna chama fulani kimehaidi kumwaga damu. Ulietuma ujumbe huu inaonesha jinsi gani ulivyo muoga kujulikana na sijui umepata wapi namba yangu? Umwagaji wa damu unaujua ni kiu gani hicho unachoongea? Mbona malori yalianguka huku yakiwa yamebeba wanachama wa chama fulani hata ujatutumia taarifa ya umwagaji wa damu zisizo na hatia? Kuna sheria gani nchini ya kubeba watu kwenye malori? Ok mi pengine uelewa wangu ni mdogo lakini sioni kama kuna uhusiano na umwagaji wa damu kama ulivyo tuma kwenye ujumbe wako.

Tafadhali waweza kunitafuta tena na kunipa habari kama una mapenzi mema na Watanzania wanaoishi katika Umasikini na wengine wakiendelea kuponda raha kwa kutumia raslimali zetu.